Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo ni siku ya ukungu duniani

Mohammed Tariq, dereva Bajaji jijini New Delhi anaeleza madhila anayokumbana nayoakiwa kazini husasani hewa chafu itakayo kwenye magari. Picha:

Leo ni siku ya ukungu duniani

Kwa mara ya kwanza dunia leo inaadhimisha siku ya ukungu ili kukumbuka watu waliopoteza maisha kutokana na athari za ukungu.

Maadhimisho haya yanafanyika ikiwa ni siku ya pili ya mkutano mkuu wa baraza la shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEA  huko Nairobi, Kenya.

Imeelezwa kuwa binadamu katika uhai wake ana vitu vingine anavyoweza kutumia au la lakini si hewa ambayo anahitaji wakati wote wa uhai wake.

Umoja wa Mataifa unasema kwa wastani kila binadamu anahitaji galoni milioni 250 za hewa katika mapafu yake ikiwa ni sawa na galoni elfu 10 za hewa kwa siku.

image
Louise Osbourne, dereva wa taxi jijini London anaelezea jinsi anavyoathiwa. Picha: UM
Hata hivyo hivi sasa hewa hiyo inakabiliwa na uchafuzi kutoka viwandani na kwenye magari ambapo baadhi ya wakazi wa miji ya London nchini Uingereza na New Delhi nchini India wameeleza vile ambavyo wanaathirika.

Mathalani ukungu kutanda hewani wanashindwa kupumua au kuona vizuri

Mohammed Tariq dereva Bajaj jijini New Delhi, India ameeleza madhila anayokumbana nayo akiwa kazini hususan hewa chafu itokayo kwenye magari na kueleza hana namna ya kujikinga nayo na lazima afanye biashara

image
Pippa Messenger(Kati), mshauri wa masuala ya maendelo jijini London ameeleza jinsia anavyoweza kukimbia umbali mrefu akiwa katika maeneo mengine lakini awapo London hawezi kukimbia zaidi ya kilometa 5. Picha: UM
Naye Pippa Messenger mshauri wa masuala ya maendelo jijini London, Uingereza ameeleza jinsia anavyoweza kukimbia umbali mrefu akiwa katika maeneo mengine lakini awapo mjini humo hawezi kukimbia zaidi ya kilometa 5 na mara nyingi hubanwa na pumu kutokana na hewa chafu inayosababisha ukungu.