Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

siku ya mazingira

05 JUNE 2020

Jaridani la Umoja wa Maitafa leo ikiwa Ijumaa ni mada kwa kina ambapo tutamulika athari za gonjwa la virusi vya Corona katika kulinda wanyama walio hatarini kutoweka.
- Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa asema tubadili tabia tulinde mazingira kwani muda unayoyoma
-  Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa leo imesema takribani watu 1,300 ambao ni raia wameuawa katika matukio tofauti nchini DRC. 
- Na shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa, IOM limesaidia raia 179 wa Mali waliokuwa wamekwama Niger.
Sauti
9'57"
UNIC/Stella Vuzo

UNEP inafungua wigo wa watu kuchangia mawazo yao kwa nini wanaona hivi sasa ni wakati wa asili-Clara Makenya

Kesho ni siku ya mazingira duniani, siku ambayo imekuwa ikiazimishwa tangu mwaka 1974 kila mwaka ifikapo tarehe 5 ya mwezi Juni. Siku hii inazihusisha serikali, wafanyabiashara, watu maarufu na wananchi  katika kuelekeza juhudi zao kwenye masuala yanayohusu mazingira hususni yle yanayotishia ustawi wa mazingira yenyewe na matokeo mabaya ya athari hizo. Mwaka huu wa 2020, kauli mbiu imejikita katika baionwai.

Sauti
3'47"

04 JUNE 2020

Jaridani la Umoja wa Maitafa leo:

- Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa asema Chanjo ni muhimu lakini pekee haitoshi

- Wakimbizi wa Mali nchini Niger wanapambana na janga la virusi vya corona kwa kutengeneza na kugawa sabuni na dawa ya kutakasa madoa baada ya kupatiwa mafunzo na UNHCR

-Mnufaika wa mafunzo ya FAO kuhusu mbinu bora za ufugaji nyuki aongea

Sauti
12'12"

Leo ni siku ya ukungu duniani

Kwa mara ya kwanza dunia leo inaadhimisha siku ya ukungu ili kukumbuka watu waliopoteza maisha kutokana na athari za ukungu.

Maadhimisho haya yanafanyika ikiwa ni siku ya pili ya mkutano mkuu wa baraza la shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEA  huko Nairobi, Kenya.

Imeelezwa kuwa binadamu katika uhai wake ana vitu vingine anavyoweza kutumia au la lakini si hewa ambayo anahitaji wakati wote wa uhai wake.