Leo ni siku ya ukungu duniani
Kwa mara ya kwanza dunia leo inaadhimisha siku ya ukungu ili kukumbuka watu waliopoteza maisha kutokana na athari za ukungu.
Maadhimisho haya yanafanyika ikiwa ni siku ya pili ya mkutano mkuu wa baraza la shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEA huko Nairobi, Kenya.
Imeelezwa kuwa binadamu katika uhai wake ana vitu vingine anavyoweza kutumia au la lakini si hewa ambayo anahitaji wakati wote wa uhai wake.