Katika siku ya kimataifa ya mabaharia IMO yataka bahari zilindwe
Leo ni siku ya kimataifa ya baharia ambayo kila mwaka huadhimishwa Juni 25 , kupitia ujumbe wake wa siku hii katibu mkuu wa shirika la kimataifa la masuala ya bahari IMO amesema mwaka huu siku hiyo inajikita katika kuainisha mchango mkubwa wa mabaharia katika usalama wa meli na ulinzi wa mazingira ya bahari.