Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukusanyaji mapato kuwezesha Somalia kubeba jukumu la ulinzi

Washiriki wa mkutano wa masuala ya ulinzi na usalama mjini Mogadishu nchini Somalia. Picha: UNSOM

Ukusanyaji mapato kuwezesha Somalia kubeba jukumu la ulinzi

Umoja wa Mataifa umetaja mambo ambayo Somalia inapaswa kuzingatia ili hatimaye iweze kubeba jukumu la ulinzi wa nchi hiyo baada ya kumaliza kwa mzozo wa wenyewe kwa wenyewe.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Michael Keating amesema hayo akihojiwa na Idhaa ya umoja huo baada ya kumalizika kwa mkutano wa masuala ya ulinzi na usalama mjini Mogadishu.

Amesema hatua ya jeshi la Somalia kushika hatamu kwenye ulinzi ni muhimu kwa kuwa vikosi vya ujumbe wa  Muungano wa Afrika, AMISOM nchini humo haviwezi kukaa maisha, hivyo..

(Sauti ya Michael Keating)

“Kunapaswa kuwepo masharti ya kipindi cha mpito kutoka AMISOM kwenda Somalia kwa kutambua kuwa AMISOM haiwezi kuwepo Somalia siku zote, imeshakuwa hapa kwa miaka 10. Na fedha kwa AMISOM iwe ni kupitia Umoja wa Mataifa au michango ya kujitolea au  Muungano wa Ulaya hiyo haiwezi kuendelea kuwepo. Lazima kuwe na ukomo.

Bwana Keating ambaye pia ni mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, UNSOM amesema tayari kuna maeneo ya viungano ambakomakabidhiano ya jukumu la ulinzi kutoka AMISOM kwenda kwa serikali ya Somalia, lakini ili kupanua wigo wake..

(Sauti ya Michael Keating)

“Kuongeza kodi ikimaanisha kupatia ulinzi sekta binafsi ili wawe tayari kulipa kodi. Pia kurejesha uhusiano wake na taasisi za kifedha duniani. Halikadhalika wasomali ni watu wajasiriamali zaidi duniani lakini ukosefu wa utulivu wa kisiasa, ukosefu wa taasisi na ukosefu wa kuaminiana vimedumaza kabisa hii na hili ni jambo ambalo tunapaswa kulishughulikia.”