Skip to main content

Chuja:

Geneva

30 MEI 2023

Jaridani hii leo ni mada kwa kina leo tunaelekea nchini DRC kuangazia kikosi cha pili cha walinda amani kutoka Kenya cha kuchukua hatua za haraka KEN QRF 2 kinachohudumu mjini Beni, Jimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, DRC-MONUSCO. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo  za matumaini kwa familia zilizokata tamaa zilizokwama katika kitovu cha mzozo nchini Sudan, msaada wa kibinadamu kwa watoto nchini humo, na wakimbizi wanaohama kwa nchi jirani.

Sauti
12'5"
Walinda amani wa Umoja wa MAtaifa kutoka Tanzania wanaohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC, MONUSCO wamesherehekea siku ya walinda amani duniani kwa kutembelea kituo cha watoto yatima huko Oicha jimboni Kivu Kaskazini.
UN News/George Musubao

DRC: Walinda amani wa UN kutoka Tanzania washerehekea siku yao kwa kutembelea watoto

Kikosi cha 10 cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, TANZBATT-10 kinachohudumu kwenye kikosi cha kujibu mashambulizi (FIB) kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kimeadhimisha siku ya ulinzi wa amani duniani hii leo tarehe 29 Mei kwa kutembelea kituo cha watoto yatima cha DORIKA kilichopo OICHA Jimbo la Kivu kaskazini nchini DRC. Wakiwa kituoni hapo wamewapatia misaada ya kiutu watoto hao ikiwa pia ni lengo la kulinda uhusiano na ushirikiano kwenye eneo lao hilo la uwajibikaji.

Takriban watu milioni 2 hadi milioni 2.5 wanatarajiwa kutumbukia kwenye janga la njaa nchini Sudan katika miezi michache ijayo.
© WFP/Peter Louis

Kuna hatari ya kuongezeka njaa - yaonya ripoti mpya ya UN 

Ripoti - 'Maeneo yenye Njaa - FAO-WFP onyo la mapema juu ya uhaba mkubwa wa chakula' - iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula (WFP) inataka hatua za haraka za kibinadamu kuokoa maisha na njia za kujikimu na kuzuia njaa na vifo katika maeneo yenye njaa kali ambayo iko katika hatari kubwa ya kuongezeka kuanzia Juni hadi Novemba 2023.