Skip to main content

Chuja:

mogadishu

Mojawapo ya picha kutoka maktaba ikionesha shambulio la kigaidi kwenye hoteli ya Benadir huko Mogadishu Somalia tarehe 25 Agosti mwaka 2016.
UN Somalia

Shambulizi la kujitoa muhanga Somalia, Umoja wa Mataifa walaani

Stéphane Dujarric ambaye ni Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa hii leo akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya UN amesema Shirika hilo linalaani shambulizi la kujitoa muhanga lilitokea leo katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, akiongeza kusema, tunatoa "rambirambi zetu kwa familia za waathiriwa," na akawatakia ahueni ya haraka wale wote waliojeruhiwa. 

Somalia yaendesha kampeni dhidi ya Surua

Nchini Somalia, mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa ushirikiano na serikali wamehitimisha kampeni ya siku tano ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa Surua iliyolenga watoto milioni 4.2 nchini kote.

Watoto hao ni wale wenye umri wa kati ya miezi 6  hadi miaka 10 ambapo kampeni hiyo inafuatia visa zaidi ya elfu 23 vilivyoripotiwa mwaka jana, idadi ambayo ni kubwa kulinganisha na miaka iliyotangulia.

Mwakilishi wa shirika la afya ulimwenguni, WHO nchini Somalia, Ghulam Popal amesema ni kipaumbele cha shirika lake kuendelea kusaidia serikali ili kudhibiti mlipuko wa surua.

Muziki waeneza amani Somalia

Kwa zaidi ya miongo miwili sasa, Somalia imeghubikwa na migogoro ikiwemo mashambulizi ya Al-Shabaab na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, na hivyo kusababisha maelfu ya raia  kupoteza maisha, makazi na wengine kusaka hifadhi nchi jirani. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa usaidizi nchini humo, UNSOM, kwa kushirikiana na serikali unatumia njia mbalimabli kuhakikisha mkataba wa amani umetekelezwa ili  watu waweze kurejea makwao. Je ni mbinu gani zinatumika kuchagiza amani? Joshua Mmali anaangazia kupitia makala hii.