Ujumbe wa Umoja wa Mataifa umeendelea na mfululizo wa ziara zake katika majimbo yanayounda serikali ya shirikisho, Somalia. Ujumbe huo ukiongozwa na Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na ambaye pia ni Mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia UNSOM, Bwana James Swan, wametembelea jimbo la Galmudug kujadiliana na uongozi jinsi Umoja wa Mataifa unavyoweza kusaidiana nao.