Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwakilishi wa Syria kushiriki mkutano wa baraza la usalama Geneva

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria Staffan de Mistura akihutubia kwa njia ya video kutoka Geneva, Uswisi (Picha:UN/Kim Haughton)

Mwakilishi wa Syria kushiriki mkutano wa baraza la usalama Geneva

Mkutano wa nadra wa wajumbe watano wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa utafanyika Geneva Uswis katika siku ya ufunguzi wa duru mpya ya mazungumzo ya amani ya Syria, amesema leo mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria Staffan de Mistura.

Akizungumza kwa njia ya video kwenye kikao cha baraza la usalama la Umoja wa mataifa kilichofanyika  kwenye makao makuu mjini New York akiwa Geneva, Bwana de Mistura amethibitisha kwamba amealikwa kwenye mkutano huo utakaofanyika kesho Jumanne.

Hatua hiyo imefikiwa wakati machafuko yaliyokatili maisha ya maelfu ya watu na kutawanya mamilioni yakiendelea Syria. De Mistura ameweka bayana changamoto zinazoikabili timu yake katika siku zijazo lakini pia fursa ya kuanza ukurasa mpya kwa maelfu ya raia walioghubikwa na vita.

(DE MISTURA CUT)

“Mgogoro huu ni moja ya mibaya zaidi katika historia ya Umoja wa Mataifa, sasa kuna fursa, fursa hasa ya kuelekea katika mchakato wa kisiasa …tunaona kuibuka kwa muafaka wa kimataifa na ni lazima tuanze kusongesha mchakato uzae matunda ili kuwawezesha Wasyria kuamua mustakhbali wao kwa uhuru.”

image
Raia waliotawanywa na ISIL wanakumbwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa dawa za kudhibiti magonjwa. Picha: WHO Syria
Ameongeza kuwa baada ya miaka sita ya vita machafuko yamepungua kwa kiasi kikubwa katika majimbo mbalimbali ya Syria akishukuru kuwepo kwa maeneo ya upunguzaji ghasia yaliyowezekana kwa hakikisho la Urusi, Uturuki na Iran. Hata hivyo amesema bado kuna maeneo yanakabiliwa na changamoto kama Ghouta Mashariki nje ya mji mkuu Damascus ambako kuna hali mbaya ya kibinadamu.

Mkutano huo wa kesho wa  wa baraza la usalama Geneva umeitishwa na Ufaransa.