Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utapiamlo wazidi kuwa “mwiba” kwa watoto Syria.

Mama mkimbizi wa ndani Syria amnawia mkono mtoto mkono. Picha: UNHCR

Utapiamlo wazidi kuwa “mwiba” kwa watoto Syria.

Vita, kukosekana kwa misaada ya kibinadamu na kupanda kwa gharama za chakula kumesababisha kuongezeka kwa kiwango cha utapiamlo nchini Syria.

Uchunguzi uliofanywa na shirika la watoto kuhudumia watoto la duniani UNICEF katika maeneo 27 mashariki mwa GHOUTA nchini Syria, umebaini kiwango kikubwa cha utapiamlo kuwahi kurekodiwa katika nchi hiyo.

Mwakilishi wa UNICEF kanda ya Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati Geert Cappelaere amesema ni lazima kuondoa vikwazo vya usambazaji misaada ya kibinadamu ili wakazi wa maeneo hayo waweze kusaidiwa kuondokana na tatizo hilo hususani kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 5.

Tangu kuanza kwa machafuko nchini Syria mwezi machi mwaka 2011zaidi ya watu laki 4 na nusu, miongoni mwao wakiwa ni watoto wamenasa katika eneo la GHOUTA kutokana na vita inayoendelea.