Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Harakati dhidi ya dondakoo zaendelea Cox Bazar

Mtoto wa kabila la Rohingya baada ya kupatiwa matibabu dhidi ya ugonjwa wa donkakoo huko Cox's Bazar nchini Bangladesh. (Picha:IOM)

Harakati dhidi ya dondakoo zaendelea Cox Bazar

Huko Bangladesh kwenye wilaya ya Cox Bazar kampeni ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa dondakoo inaendelea kwa wakimbizi kutoka Rohingya. Taarifa zaidi na Joseph Msami.

(Taarifa ya Joseph Msami)

Shirikala afya ulimwenguni WHO linasema takwimu za karibuni zaidi zinaoyesha watu zaidi ya 2500 wameambukizwa ugonjwa huo ambapo kati yao hao 27 wamefariki dunia.

Ugonjwa huo wa dondakoo unaoenezwa na bakteria husababisha mgonjwa kuvimba koo kiasi kwamba hawezi kuvuta pumzi wala kumeza chakula.

Tayari WHO na wadau wake wametenga eneo maalum la matibabu kwenye kambi ya wakimbizi  ya Kutupalong na utoaji chanjo ambapo mmoja wa wagonjwa Muhamad anasema katu hajawahi kufahamu ugonjwa huo.

Pamoja na chanjo, wagonjwa wanapatiwa ushauri nasaha hasa kwa kuzingatiwa wanapotengwa na familia zao wanakumbwa na kiwewe.

Jonathy Polonsky ni mtaalamu wa magonjwa kutoka WHO huko Cox Bazar anazungumzia kile kinafanyika ili kuzuia kuenea kwa magonjwa na matumizi ya mwongozo wa matibabu.

(Sauti ya Jonath Polonsky)

“Tumeandaa muongozo na sasa tuko kwenye mchakato wa kutoa mafunzo ya jinsi ya kutumia. Lakini zima tubaini, tuwatenge na tuwatibu mtu yeyote ambaye amekuwa na magusano na mgonjwa yoyote wa dondakoo ili kupunguza hatari kwa jamii.  Tuna uwezo wa kutibu ugonjwa huu kwa hiyo suluhisho bora ni kuwabaini mapema na kuwapatia matibabu.”