Utoweshwaji Bangladesh: Türk ataka haki na uwazi katika kesi
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu, Volker Türk, amesema leo kuwa kuanzishwa kwa mashitaka rasmi dhidi ya watuhumiwa wa utekaji nyara na mateso chini ya utawala uliopita nchini Bangladesh ni hatua muhimu kuelekea uwajibikaji.