Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.
Taarifa kuhusu Virusi vya Corona
Homa ya kichomi huwaacha Watoto milioni 4.2 wakihaha bila oksijeni kila mwaka:Ripoti
Tathimini mpya iliyotolewa leo na mashirika ya kimataifa ukiwemo Umoja wa Mataifa imesema takribani watoto milioni 4.2 wa chini ya umri wa miaka mitano wanaathirika na uhaba wa hewa ya oksjeni kutokana na homa kali ya kichomi au pneumonia.
COVID-19 yaathiri wahamiaji na utumaji fedha nyumbani
Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imebaini kuwa viwango vya njaa na ukimbizi ambavyo tayari vilikuwa vimevunja rekodi kabla ya mlipuko wa wa ugonjwa wa Corona au COVID-19, vitazidi kuongezeka wakati huu ambapo wahamiaji na wategemezi wa fedha kutoka nje wanahaha kusaka kazi ili kusaidia familia zao.
Njia pekee ya kupambana na janga hili ni kuhakikisha chanjo inapatikana kwa gharama nafuu kwa kila mtu dunian-UN
Wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo wamezikosoa nchi zinazojaribu kubinafsisha na kuhodhi chanjo yoyote ya dhidi ya corona au COVID-19 inayotarajiwa kupatikana wakisema njia pekee ya kupambana na janga hili ni kuhakikisha chanjo inapatikana kwa gharama nafuu kwa kila mtu duniani.
Hifadhi ya Dja Cameroon yachukua hatua kupambana na COVID-19
Maeneo mengi ya hifadhi za viumbe hai na misitu pamoja na mbuga za wanyama pori yameathirika kwa namna moja au nyingine kutokana na uwepo wa mlipuko vya virusi vya corona ulimwenguni. Hifadhi ya Dja nchini Cameroon ni miongoni mwa waathirika, lakini ambao wanafanya chini juu kujikinga na kujikwamua na hali hiyo.
Hakuna mtu atakayekuwa salama hadi wote watakapokuwa salama dhidi ya COVID-19:UN
Wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo wamezikosoa nchi zinazojaribu kubinafsisha na kuhodhi chanjo yoyote ya dhidi ya corona au COVID-19 inayotarajiwa kupatikana wakisema njia pekee ya kupambana na janga hili ni kuhakikisha chanjo inapatikana kwa gharama nafuu kwa kila mtu duniani.
Kando na madhila yatokanayo na COVID-19 kwa upande mwingine imetoa fursa ya ubunifu
Utafiti mpya wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO uliotangazwa katika mji mkuu wa Jamhuri ya Congo, Brazzaville, umesema janga la COVID-19 limeongeza nguvu kwenye maendeleo ya ubunifu zaidi ya 120 wa teknolojia ya afya ambao umejaribiwa au kupitishwa barani Afrika.
COVID-19 inahimiza ubunifu wa kiafya barani Afrika-WHO
Utafiti mpya wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO uliotangazwa katika mji mkuu wa Jamhuri ya Congo, Brazzaville, umesema janga la COVID-19 limeongeza nguvu kwenye maendeleo ya ubunifu zaidi ya 120 wa teknolojia ya afya ambao umejaribiwa au kupitishwa barani Afrika.
Mashahiri yatumika kupinga ukatili kwa watoto miongoni mwa wakimbizi Uganda wakati wa COVID-19
Kufuatia mlipuko wa COVID-19 mnamo Machi mwaka huu nchini Uganda, shule zilifungwa na hivyo kuwaweka hatarini watoto kukumbana na ukatili wa kijinsia hasa katika makazi ya wakimbizi ambako huduma nyingi huwa hazitoshelezi jamii hizo. Kwa mantiki hiyo, shirika la Umoja wa Mataifa kupitia wadau wake wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali kuhamasisha jamii kuhakikisha ulinzi wa watoto wa kike na wale wa kiume. Sasa, watoto wenyewe wanashirikishwa katika kampeni ya kuwalinda kwa kuwapatia nafasi ya kuzungumzia changamoto na mikakati ya kuzikabili.
Dunia iko katika janga la tsunami ya COVID-19: Guterres
Ikiwa leo ni siku ya uelimishaji kuhusu tsunami duniani Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameitaka dunia kuiba uzoefu wa maandalizi ya majanga kwenye hatua zilizopigwa katika kupunguza vifo vitokanavyo na tsunami.
WHO na mbinu kabambe kukabiliana na COVID-19 Lebanon
Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO linatoa msaada wa aina mbalimbali kusaidia vita dhidi ya janga la corona au COVID-19 nchini Lebanon hasa kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa baada ya milipuko iliyotokea mwezi Agosti mwaka huu mjini Beirut.