Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashahiri yatumika kupinga ukatili kwa watoto miongoni mwa wakimbizi Uganda wakati wa COVID-19  

Mashahiri yatumika kupinga ukatili kwa watoto miongoni mwa wakimbizi Uganda wakati wa COVID-19  

Pakua

Kufuatia mlipuko wa COVID-19 mnamo Machi mwaka huu nchini Uganda, shule zilifungwa na hivyo kuwaweka hatarini watoto kukumbana na ukatili wa kijinsia hasa katika makazi ya wakimbizi ambako huduma nyingi huwa hazitoshelezi jamii hizo. Kwa mantiki hiyo, shirika la Umoja wa Mataifa kupitia wadau wake wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali kuhamasisha jamii kuhakikisha ulinzi wa watoto wa kike na wale wa kiume. Sasa, watoto wenyewe wanashirikishwa katika kampeni ya kuwalinda kwa kuwapatia nafasi ya kuzungumzia changamoto na mikakati ya kuzikabili. 

Je, wanafanya nini? Basi ungana na John Kibego kutoka Uganda katika makala ifuatayo kwa maelezo zaidi. 

Audio Credit
Grace Kaneiya/ John Kibego
Sauti
3'29"
Photo Credit
© UNHCR/Rocco Nuri