Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hifadhi ya Dja Cameroon yachukua hatua kupambana na COVID-19 

Hifadhi zinachukua hatua kukabiliana na COVID-19 na kuhakikisha utalii salama.Simba katika hifadhi ya Masai Mara nchini Kenya
UNEP GRID Arendal/Peter Prokosch
Hifadhi zinachukua hatua kukabiliana na COVID-19 na kuhakikisha utalii salama.Simba katika hifadhi ya Masai Mara nchini Kenya

Hifadhi ya Dja Cameroon yachukua hatua kupambana na COVID-19 

Afya

Maeneo mengi ya hifadhi za viumbe hai na misitu pamoja na mbuga za wanyama pori yameathirika kwa namna moja au nyingine kutokana na uwepo wa mlipuko vya virusi vya corona ulimwenguni. Hifadhi ya Dja nchini Cameroon ni miongoni mwa waathirika, lakini ambao wanafanya chini juu kujikinga na kujikwamua na hali hiyo.

Hapa ni katika hifadhi ya wanyamapori na viumbe hai vingine ya Dja, iliyoko kusini mashariki mwa Cameroon. Kama zilivyo hifadhi nyingine kote duniani, athari za COVID-19 ni dhahiri lakini mapambano dhidi ya ugonjwa huo nayo ni dhahiri.  

Katika hifadhi hii ambayo shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO liliifanya kuwa moja ya urithi wa dunia mnamo mwaka 1987, wahifadhi wamejipanga na wanachukua tahadhari zote.  

 “Mipangilio kadhaa imefanywa kwa ajili ya uhifadhi wa hifadhi hii ya Dja kupambana na COVID-19.” Anasema mmoja wa maafisa wa hifadhi hii.  

Afisa mwingine akionesha vifaa vya kusafisha mikono walivyovisambaza kila maeneo ya majengo na ofisi anaeleza akisema, “ kote katika majengo na ofisi za kutolea huduma, tumeweka vifaa vya kutunzia maji vyenye koki, sabuni na vitakasa mikono kawa ajili ya kusafishia mikono. Tumehitaji uvaaji wa barakoa kwa watumiaji wote na maafisa wa kitengo cha uhifadhi. Tunapanga kazi kulingana na mzunguko wa utunzaji wa wafanyakazi wote.”  

Kuhusu kuokoa viumbe na watalii katika hifadhi Afisa huyu anasema,“kuingia katika hifadhi kumesitishwa kwa watalii na watafiti. Tunafanya kampeni za kuelimisha ndani ya jamii zilizo kandokando mwa hifadhi na tunaendelea kupambana na uwindaji haramu na pia kufuatilia ikolojia kwa hatua za usalama.”