Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.
Taarifa kuhusu Virusi vya Corona
Guterres: Tutumie siku ya afya duniani kuboresha mifumo ya afya
Kuelekea siku ya afya duniani kesho tarehe 7 mwezi Aprili, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametilia mkazi maudhui ya mwaka huu ya siku hiyo ya afya ambayo ni kujenga dunia ya usawa zaidi na yenye haki, kwa kuzingatia jinsi janga la COVID-19 limefichua ukosefu wa usawa na haki kwenye mifumo ya afya. Taarifa ya Jason Nyakundi inaeleza zaidi.
05 APRILI 2021
Ugonjwa wa Corona au COVID-19 ulizua zahma kubwa duniani ulipoibuka mwaka jana na kuleta sintofahamu. Hali hiyo bado haijaisha hadi sasa ambapo ni mwaka mmoja umeshapita na watu zaidi ya milioni 128 wameugua duniani kote hadi sasa na kati yao hao zaidi ya milioni 2.8 wamefariki dunia. Bado mazuio ya safari yamewekwa katika baadhi ya nchi na masharti ya kujikinga kwa kuvaa barakoa, kuepuka michangamano na kutumia vitakasa mikono zinazingatiwa. Hata hivyo chanjo imepatikana na inaleta nuru.
Utoaji chanjo ya COVID-19 barani Ulaya uko katika kasi isiyokubalika: WHO
Utoaji wa chanjo za COVID-19 barani Ulaya unaenda kwa mwendo wa polepole usiokubalika wakati maambukizi mapya yakiongezeka katika makundi yote, hiyo ni kwa mujibu wa ofisi ya shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO kanda ya Ulaya ambayo inashughulikia nchi na himaya 53.
WHO yaondoa hofu kuhusu chanjo ya AstraZeneca na kuidhinisha ya Jonhson & Jonson
Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO limesema leo kwamba linajua kuhusu hofu ya damu kuganda inayohusishwa na kundi maalum la chanjo ya AstraZeneca-Oxford dhidi ya gonjwa la corona au COVID-19, lakini inashikilia kuwa hadi sasa, hakuna mtu aliyekufa kutokana na chanjo yoyote dhidi ya virusi vya corona .
Mwaka mmoja wa janga la COVID-19 kuna nuru gizani:Guterres
Baada ya miezi 12 ya ulimwengu kukabiliwa na "tsunami ya mateso", kuwasili kwa chanjo dhidi ya janga la corona au COVID-19 inashiria nuru fulani baada ya kiza totoro" amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo Alhamisi,ikiwa ni maadhimisho yam waka mmoja tangu shirika la afya la Umoja wa Mataifa (WHO) ) kutangaza rasmi kuwa janga hilo ni la kimataifa.
Vijana wa kike wahimizwa kupigania haki za kumiliki ardhi Uganda.
Wiki hii dunia ikiwa imeadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake duniani ambapo sehemu mbalimbali wanawake waliitumia kuonesha kero zao na kutiana moyo. Nchini Uganda, wanawake katika wilaya ya Buliisa wameandamana hadi Makao Makuu ya wilaya hiyo kuwasilisha malalamiko yao wakiitaka serikali ishughulikie changamoto yao ya kunyimwa haki ya kumiliki ardhi.
Watu 1,600 wamechanjwa dhidi ya Ebola Guinea, chanjo zaidi zahitajika: WHO
Watu zaidi ya 1,600 wameshapokea chanjo dhidi ya virusi hatari vya Ebola ambako shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO linasema watu wanne wamepoteza maisha kufuatia mlipuko mpya wa ugonjwa.
Theluthi 2 ya mwaka wa masomo duniani imepotea sababu ya COVID-19:UNESCO
Ikiwa ni mwaka mmoja sasa tangu kuzuka kwa janga la corona au COVID-19, Zaidi ya wanafunzi milioni 800 ambao ni zaidi ya nusu ya wanafunzi wote duniani bado wanakabiliwa changamoto kubwa ya kuvurugwa kwa elimu yao, kuanzia kufungwa kwa shule katika nchi 31 hadi kupunguzwa au kusoma kwa muda mfupi katika nchi zingine 48 kwa mujibu wa takwimu mpya zilizotolewa leo kupitia ramani ya ufuatiliaji ya shirika la Umoja wa Mataifa la elimu na utamaduni UNESCO.
Chanjo ya COVID-19 yaanza kutolewa kwa wakimbizi nchini Jordan
Wakimbizi nchini Jordan wameanza kupokea chanjo ya COVID-19 ikiwa ni sehemu ya mpango wa kitaifa wa afya ambao unajumuisha raia wote, wakimbizi na wakazi.
06 JANUARI 2021
Katika Jarida la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea
- Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito wa kuhakikisha mizozo inasitishwa na mizizi yake kukatwa kwa lengo la kudumisha amani na kufikia ajenda ya maendeleo ya 2030 hususan brani Afrika.
-Walinda amani kutoka Burundi, Bangladesh na Cameroon waliopoteza maisha Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR wakati wa Krisimasi waagwa na kusafirishwa makwao kwa maziko