Shambulio la Urusi kwenye eneo la manunuzi Ukraine halikubaliki- UN
Huko Ukraine hii leo imeripotiwa ya kwamba shambulio lililofanywa na jeshi la Urusi kwenye eneo la manunuzi lenye watu wengi mjini Kharkiv limesababisha vifo vya takribani watu wanne. Denise Brown, Mratibu wa Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Ukraine amelaani vikali shambulio hilo na kutaka raia walindwe.