Gaza : ICJ imeitaka Israel kukomesha mashambulizi dhidi ya Rafah mara moja
Gaza : ICJ imeitaka Israel kukomesha mashambulizi dhidi ya Rafah mara moja
Mahakama ya kimataifa ya haki ICJ leo imetoa maamuzi ya kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel iliyowasilishwa Mei 10 ikiitaka ICJ kuiamuru Israel isitishe mara moja oparesheni zake zote za kijeshi na kuwezesha upatikanaji wa misaada ya kibinadamu. Na tarehe 16 na 17 Mei,kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari katika Ukanda wa Gaza.
Maagizo ya ICJ, ambayo huamua mizozo kati ya nchi ni ya kisheria lakini haina njia ya kuyatekeleza.
Agizo la leo la ICJ linakuja siku chache baada ya Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC Karim Khan kuomba hati ya kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, Waziri wake wa Ulinzi Yoav Gallant, na viongozi watatu wa Hamas, kwa madai ya uhalifu uliofanywa huko Gaza na Israel.
Hali mbaya ya kibinadamu
Katika agizo lake, Mahakama ya Kimataifa ya Haki imesisitiza kwamba “hali ya janga la kibinadamu katika Ukanda wa Gaza, ambayo ilibainisha katika agizo lake la Januari 26, 2024, inaelekea kuzorota, wakati huo huo kuporomoka hata zaidi tangu ilipotoa agizo lake la Machi 28, 2024.”
Mahakama inaona kwamba maendeleo haya, ambayo ni makubwa sana, yanajumuisha "mabadiliko ya ya maana hali ndani ya Kifungu cha 76 cha Kanuni".
Ni zaidi ya maoni kwamba hatua za tahadhari zilizoainishwa katika agizo lake la Machi 28, 2024, pamoja na zile zilizothibitishwa tena, hazijumuishi kikamilifu matokeo yanayotokana na mabadiliko haya ya hali, ambayo yanahalalisha marekebisho ya hatua hizi.
Mahakama pia inaona kwamba, kulingana na taarifa zinazopatikana, "hatari kubwa zinazohusiana na mashambulizi ya kijeshi huko Rafah zimeanza kuwa ukweli, na zitaongezeka zaidi ikiwa operesheni itaendelea."
Ikikabiliwa na hali hii, katika amri yake ya leo Ijumaa, Mei 24, Mahakama inathibitisha, kwa kura 13 kwa mbili, hatua za muda zilizoainishwa katika amri zake za Januari 26 na Machi 28, 2024, ambazo lazima zitekelezwe mara moja na kwa ufanisi.
Hatua mpya za tahadhari
Kwa kura 13 kwa mbili, ICJ pia imetaja hatua mpya za tahadhari kwamba taifa la Israeli, kwa kuzingatia wajibu wake chini ya Mkataba juu ya Kuzuia na Adhabu ya Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari, na kwa kuzingatia hali mbaya ya maisha inayowakabili raia katika Jimbo la Rafah
, "Sitisha mara moja uvamizi wake wa kijeshi, na hatua nyingine yoyote itakayofanywa katika mkoa wa Rafah, ambayo inaweza kuwaweka kundi la Wapalestina huko Gaza katika hali ya kuishi ambayo inaweza kuleta uharibifu kamili au sehemu.
Kwa kura kumi na tatu kwa mbili, Mahakama inaonyesha kwamba Jimbo la Israeli lazima “kuweka kivuko cha Rafah wazi ili utoaji wa huduma za msingi na misaada uweze kuhakikishwa, bila kizuizi na kwa kiwango kikubwa ilihitaji msaada wa haraka wa kibinadamu.
Kwa kura 13 kwa mbili mahama imeitaka Israel, kuchukua hatua madhubuti ili kuhakikisha ufikiaji usiozuiliwa wa Ukanda wa Gaza kwa tume yoyote ya uchunguzi, ujumbe wa kutafuta ukweli au chombo kingine cha uchunguzi kilichoagizwa na vyombo vyenye uwezo wa Umoja wa Mataifa kuchunguza tuhuma za mauaji ya kimbari;
Kwa kura kumi na tatu kwa mbili, ICJ inaamua kwamba kwamba Israeli itawasilisha ripoti kwa Mahakama juu ya hatua zote kuchukuliwa ili kutekeleza agizo hili, ndani ya mwezi mmoja kuanzia tarehe ya agizo hili.
Maamuzi ya ICJ yana mashiko, anakumbusha Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, kupitia msemaji wake, Stéphane Dujarric amesema amezingatia agizo la ICJ, lililotolewa leo huko The Hague Uholanzi.
"Katibu Mkuu amekumbuka kwamba, kwa mujibu wa Mkataba na Sheria ya Mahakama, maamuzi ya Mahakama ya Kimataifa yanabana na anatumai wahusika watatii amri ya Mahakama," alisema msemaji huyo na kuongeza kwamba "Kwa mujibu wa Mkataba wa Mahakama, Katibu Mkuu pia atawasilisha haraka iwezekanavyo kwa Baraza la Usalama taarifa ya hatua za muda zilizoamriwa na Mahakama."
PHOTO
Afrika Kusini: Gaza imekuwa magofu
Akiwasilisha hoja za nchi yake Mei 16, balozi wa Afrika Kusini nchini Uholanzi, Vusimuzi Madonsela, alisema nchi yake ililazimika kurejea Mahakamani kutokana na wajibu wake chini ya Mkataba wa Mauaji ya Kimbari.
"Kutokana na kuendelea kuangamizwa kwa watu wa Palestina, huku zaidi ya watu 35,000 wakiuawa na sehemu kubwa ya Gaza ikiwa magofu. Imebidi tuwajibike."
Naye Vaughn Lowe, wa kundi la wanasheria na wataalam wanaowasilisha hoja hizo kwa upande wa Africa Kusini amesema "Jambo muhimu leo ni kwamba lengo la Israel la kuifuta Gaza kwenye ramani liko karibu kutimia. Ushahidi wa uhalifu wa kutisha na ukatili unaharibiwa kirahisi na kuwapa fursa ya wazi wale waliofanya uhalifu huu na kufanya dhihaka dhidi ya haki."
Israeli: Ukandamizaji mchafu
Akiwa mbele ya Mahakama mnamo Mei 17, Gilad Noam, mshirika mwenza wa Israel, alikanusha madai ya Afrika Kusini na kusema ni “matumizi mabaya ya Mkataba mtakatifu zaidi wa Mauaji ya Kimbari.”
Alitangaza kuwa Israel inahusika katika mzozo wa silaha "mgumu na wa kutisha", jambo muhimu ni "kuelewa hali” lakini inapuuzwa na Afrika Kusini. "Inafanya mzaha kwa tuhuma mbaya za mauaji ya kimbari, ukweli ni muhimu na ukweli unapaswa kuwa muhimu."
Maneno lazima yahifadhi maana yake. “Kuita kinachoendelea kuwa mauaji ya kimbari tena na tena hakufanyi kuwa ni mauaji ya kimbari,” aliongeza.
Ombi la Afrika Kusini 29 Desemba
Ombi lililowasilishwa Mei 10 na Afrika Kusini linahusiana na kesi inayoendelea ya Afrika Kusini inayoishutumu Israel kwa kukiuka majukumu yake chini ya Mkataba wa Mauaji ya Kimbari.
Tarehe 29 Desemba 2023, Afrika Kusini iliwasilisha ombi la kuanzisha kesi dhidi ya Israeli kuhusu madai ya Serikali hiyo kushindwa kutimiza wajibu wake chini ya Mkataba wa Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari kuhusiana na hili. ambayo inawahusu Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
Ombi hilo pia lilikuwa na ombi la dalili ya hatua za muda za "kulinda dhidi ya madhara makubwa zaidi na yasiyoweza kurekebishwa ya haki ambazo watu wa Palestina wanazo chini ya Mkataba wa Mauaji ya Kimbari, na kutaka kuheshimiwa na Israeli kwa majukumu yake chini ya Mkataba huo kwa kutotekeleza mauaji ya kimbari pamoja na kuzuia na kuadhibu mauaji ya kimbari.”
Kusikilizwa kwa kesi ya ombi hilo la Afrika Kusini kuilifanyika hadharani Januari 11 na 12, 2024.
Na Januari 26, 2024, Mahakama ya Kimataifa ya Haki ilitoa amri ya hatua za muda za kuzuia madhara yoyote kwa wakazi wa Gaza.
Hata hivyo, hakukuwa na wito wa kusitishwa mara moja kwa operesheni kubwa za