Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua za mapema dhidi ya hali ya hewa zina manufaa

Amina Hakizimana aliokoa nyumba yake kutokana na mafuriko makubwa ya Burundi kwa pesa taslimu za WFP ambazo zilienda kuimarisha nyumba yake.
© WFP/Irenee Nduwayezu
Amina Hakizimana aliokoa nyumba yake kutokana na mafuriko makubwa ya Burundi kwa pesa taslimu za WFP ambazo zilienda kuimarisha nyumba yake.

Hatua za mapema dhidi ya hali ya hewa zina manufaa

Tabianchi na mazingira

Kupitia mipango ya mapema, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na wadau wake wanapunguza athari za hali mbaya ya hewa katika nchi zinazokabiliana na njaa.

Katika jimbo la Rumonge kusini mwa Burundi, Amina Hakizimana alikwepa mafuriko makubwa yaliyopiga kijiji chake kutokana na ujumbe wa tahadhari za mapema na msaada wa fedha kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) uliomuwezesha kuimarisha nyumba yake. 

Zaidi ya kilomita 2,000 mbali katika Kusini mwa Africa, WFP ilitoa mbegu zinazostahimili ukame, mbolea na visima kwa wakulima wa Zimbabwe kama Ledinah Muzamba, ambao wanakabiliana na mojawapo ya ukame mkali zaidi katika miongo kadhaa. Kwingineko, ukuta wa ulinzi uliodhaminiwa na WFP uliokoa wanakijiji pamoja na mazao kutokana na mafuriko hatari ya ghafla yaliyoharibu sehemu za Afghanistan.

Mifano hii mitatu inajumuisha sura tofauti za majanga ya mabadiliko ya tabianchi na El Niño, joto la asili la katikati na mashariki mwa Pasifiki ambalo linaweza kubadilisha hali ya hewa duniani  na njia za kuweza kutarajia athari zake kwa ufanisi zaidi.

Shamba la mahindi lililoharibiwa na ukame nchini Zambia, mojawapo ya nchi ambazo zimetangaza hali ya dharura huku likikabiliana na athari za El Niño.
© WFP/Nkole Mwape
Shamba la mahindi lililoharibiwa na ukame nchini Zambia, mojawapo ya nchi ambazo zimetangaza hali ya dharura huku likikabiliana na athari za El Niño.

Karibu mwaka mmoja tangu kufika kwake, aina hii  mpya la El Niño, pamoja na mabadiliko ya tabianchi, imesababisha madhara makubwa kwa baadhi ya jamii maskini na zilizo hatarini zaidi duniani. Lakini athari za El Niño zimepunguzwa katika matukio ambapo watu na serikali wamepokea vifaa, mafunzo, na maarifa ya kujiandaa kwa matukio ya hali mbaya ya hewa mapema. 

"Tunajua athari za El Niño na La Niña kutokana na yaliyopita, kwa hivyo tunaweza kufikiria kitakachotokea siku zijazo," anasema mkuu wa Programu za Hatua za mapema za WFP Jesse Mason, zinazowaruhusu watu na serikali kujilinda kabla athari za hali ya hewa hazijafika.

Masomo hayo ni ya muhimu zaidi leo, wakati El Niño inapodhoofika. Baada ya ‘wakati mtulivu,’ wataalamu wengi wanabashiri kuwa kinyume kikali cha El Niño, iitwayo La Niña inayoambatana na kupungua kwa joto la Pasifiki inaweza kufika mwishoni mwa mwaka huu, kubadilisha tena mifumo ya hali ya hewa. kwa mfano, Colombia tayari inakabiliwa na msimu wa mvua wa mapema na mzito isivyo kawaida. Kwa kuwa majanga ya mabadiliko ya tabianchi yanazidisha athari za hali ya hewa duniani, matukio kama haya yanazidi kuwa ya kawaida.

“Hatua za mapema na mipango haziokoi tu  serikali na wahisani mamilioni ya dola mbali pia zinajenga ustahimilivu kwa matukio ya baadaye ambazo, pia zinajenga ustahimilivu kwa matukio ya baadaye, tunahitaji kufanya zaidi kwa dharura zinazoweza kutabirika kama hizi". “hakuna sababu ya kushikwa bila kujiandaa.” anaeleza Mason.

Mkurugenzi Mtendaji wa WFP Cindy McCain aakiangalia uharibifu unaosababishwa na ukame uliokithiri wa El Niño nchini Zambia.
© WFP/Nkole Mwape
Mkurugenzi Mtendaji wa WFP Cindy McCain aakiangalia uharibifu unaosababishwa na ukame uliokithiri wa El Niño nchini Zambia.

Faida za hatua za mapema

Mwaka jana pekee, WFP iliwalinda zaidi ya watu milioni 4 katika nchi 36 kupitia mikakati ya mapema inayowaruhusu kutarajia na kuchukua hatua kabla ya matukio ya hali ya hewa. Idadi hizi zilikuwa juu sana kutoka mwaka 2022, na kunayo  mipango ya kuziongeza zaidi katika miaka ijayo.

Afrika Mashariki, ambapo mafuriko makali yameharibu maeneo ya kilimo katika nchi kadhaa, WFP inawafikia zaidi ya watu 200,000 na usaidizi wa haraka wa chakula na lishe pamoja na tahadhari na uhamishaji wa mapema wa pesa.

"Nimeishi hapa kwa miaka sita na sijawahi kuona mvua nzito kama hii," anasema Amina Hakizimana akiwa nchinini Burundi, mojawapo ya nchi zilizoathiriwa zaidi na mafuriko.

"Kwa bahati nzuri, tulipewa tahadhari na kusaidiwa mapema," anasema kuhusu takriban dola za Kimarekani 80 katika fedha za WFP alizotumia kuimarisha nyumba yake kwenye mwambao wa Ziwa Tanganyika.

Grace Mukamana mkulima nchini Rwanda hupokea taarifa kuhusu tabianchi kupitia simu yake ya kiganjani au rununu.
©IFAD/Simona Siad
Grace Mukamana mkulima nchini Rwanda hupokea taarifa kuhusu tabianchi kupitia simu yake ya kiganjani au rununu.

Utabiri wa msimu

Kabla ya mvua kuanza, WFP na Msalaba Mwekundu wa Burundi walitambua hatari na hatua za kujiandaa katika jamii zilizo hatarini. Vile vile, walitoa vifaa na mafunzo kwa Taasisi ya Jiografia ya Burundi  kuhusu njia za kuimarisha utabiri wa msimu na kusambaza ujumbe wa tahadhari za mapema kwa jamii. 

"Nashukuru kwa utabiri wa hali ya hewa wa tahadhari za mapema, sasa tunaweza kutabiri kama mvua zitakuwa nzito au nyepesi katika vipindi vijavyo," anasema Ezekiel Kayoya wa Taasisi hiyo.

Kabla ya mvua kubwa nchini Somalia, WFP ilitoa uhamisho wa fedha wa mapema kwa makumi ya maelfu ya watu walio hatarini, pamoja na ujumbe wa tahadhari za mapema kupitia redio na simu kwa karibu watu milioni 2 zaidi. 

"Tulisikiliza ujumbe na kujiandaa kabla ya mafuriko kufika, ili tuondoke karibu na maji," anasema Ruqiyo Muhumed Mohamud, ambaye anaishi katika kambi ya watu waliokimbia makazi yao katika mji wa kati wa Beledweyne, Somalia.

Pia alinunua chakula kwa takriban dola za Kimarekani 70 kutoka kwa fedha za WFP. "Hii itatosha kwangu na familia yangu wakati wa msimu wa mafuriko," anaongeza.

Mafuriko makubwa yamekumba maeneo ya Afrika Mashariki ikiwemo Burundi, karibu na Ziwa Tanganyika.
© WFP/Irenee Nduwayezu
Mafuriko makubwa yamekumba maeneo ya Afrika Mashariki ikiwemo Burundi, karibu na Ziwa Tanganyika.

Kutoka kwa mafuriko na kukumbwa na ukame

Wakati mvua kubwa zikinya  Afrika Mashariki, Kusini mwa Afrika inakabiliana na moja ya ukame mbaya zaidi kwa miaka mingi, jambo lililosababisha serikali ya Zimbabwe, kutangaza hali ya janga. 

Serikali za Kusini mwa Afrika zimechukua hatua mapema ili kupunguza madhara, anasema mtaalamu wa WFP Mason. “Kila serikali ina huduma ya kitaifa ya hali ya hewa na  wanajua jinsi hali ya hewa ilivyo muhimu, thamani iliyoongezwa na WFP ni kuunganisha hayo na watu walio hatarini” anaongeza Mason.

Nchini Zimbabwe ambako wengi wanakabiliwa na ukosefu wa uhakika wa chakula. (Maktaba)
WFP/Tatenda Macheka
Nchini Zimbabwe ambako wengi wanakabiliwa na ukosefu wa uhakika wa chakula. (Maktaba)

“Katika wilaya ya Binga magharibi mwa Zimbabwe, kwa mfano, WFP inatoa mbegu zilizo na uwezo wa kustahimili ukame, huku ikiwafundisha jamii jinsi ya kutumia taarifa za hali ya hewa, na kuchimba visima ili kupata maji ya kutumia kwa mazao, mifugo na watu.

“Tutaweza kulima bustani katika jamii yetu na pia kuwa na maji kwa ajili ya ng'ombe wetu, tumekuwa tukisafiri umbali mrefu kupata maji kwa ajili ya ng'ombe wetu ,kilomita nyingi .” anasema mkulima wa Binga Ledinah Muzamba.