Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Rais wa Baraza Kuu la UN Balozi Dennis Francis akiwapatia waandishi wa habari tathmini ya vikao vya ngazi ya juu vya mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la UN (UNGA78).
UN /Eskinder Debebe

SDGs zilikuwa 'mdomoni' mwa kila mtoa hotuba – Rais UNGA78

Kile nilichoshuhudia ni jamii ya kimataifa iliyojizatiti upya kukamilisha utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ifikapo mwaka 2030, amesema Rais wa Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA78, Dennis Francis akizungumza na waandishi wa habari, ikiwa ni mara ya kwanza tangu ashike wadhifa huo.

Dkt. Bonifasi Masawe,  akiwaonyesha hatua kwa hatua washiriki, ripoti ya utafiti ulio fanywa wa upimaji udongo.
UN News/John Kabambala

FAO Tanzania na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine wapima udongo katika wilaya 6 Tanzania

Kilimo ni nguzo muhimu ya uchumi na chanzo kikuu cha chakula. Kupata mazao bora na mavuno mengi kunategemea sana ubora wa udongo. Hatua hizi zikichukuliwa kila pembe ya dunia kutasaidia wakulima kuelewa mchanganyiko wa madini na virutubisho katika udongo wao, linaelimisha shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO.

Sauti
5'59"
Mradi wa FAO nchini Thailand wa kupunguza upotevu wa chakula na taka kuna jukumu muhimu katika kubadilisha mifumo ya kilimo na chakula.
© FAO/Alisa Suwanrumpha

Mradi wa FAO wa kupunguza upotevu na utupaji wa chakula nchini Thailand wainua kipato cha wafanyabiashara

Kupunguza upotevu na utupaji wa chakula kuna jukumu muhimu katika kubadilisha mifumo ya kilimo na chakula. Kati ya malengo 17 ya Maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa ambayo yanafikia kilele mwaka 2030 lengo namba 2 linahimiza kutokomeza njaa, lengo namba 8 linahimiza kazi nzuri na ukuaji wa kiuchumi na lengo namba 12 lina himiza utumiaji na uzalishaji wenye kuwajibika lengo likiwa kuwa na mifumo endelevu ya utumiaji wa rasilimali. Malengo yote haya yanaenda sambamba na harakati za kupunguza upotevu na utupaji wa chakula.