Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO Tanzania na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine wapima udongo katika wilaya 6 Tanzania

Dkt. Bonifasi Masawe anaelezea ripoti ya utafiti wa upimaji wa udongo kwa washiriki katika mkutano katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine nchini Tanzania.
UN News/John Kabambala Dkt. Bonifasi Masawe, akiwaonyesha hatua kwa hatua washiriki, ripoti ya utafiti ulio fanywa wa upimaji udongo.

FAO Tanzania na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine wapima udongo katika wilaya 6 Tanzania

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Kilimo ni nguzo muhimu ya uchumi na chanzo kikuu cha chakula. Kupata mazao bora na mavuno mengi kunategemea sana ubora wa udongo. Hatua hizi zikichukuliwa kila pembe ya dunia kutasaidia wakulima kuelewa mchanganyiko wa madini na virutubisho katika udongo wao, linaelimisha shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO.

Kwa kujua hali ya udongo wao, wakulima wanaweza kuchagua mazao yanayofaa zaidi na kutumia mbolea sahihi kwa kuzingatia mahitaji ya udongo. Hii husaidia kuongeza uzalishaji na kuboresha maisha yao. Kando na faida hizo, upimaji wa udongo unasaidia kuzuia uharibifu wa ardhi na uchafuzi wa mazingira kwa kuzuia matumizi mabaya ya mbolea na kemikali.

Kundi la washiriki kutoka FAO Tanzania na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine wakipiga picha katika hafla ya elimu kwa umma kuhusu udongo nchini Tanzania.
UN News/John Kabambala FAO Tanzania na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine waelimisha umma kuhusu udongo katika wilaya 6 Tanzania.

FAO Tanzania kwa kushirikiana na wadau imewezesha hatua hiyo kufanyika kwa upimaji wa udongo katika Wilaya sita kwenye mikoa sita ambako mradi wa kulinda na kuhifadhi baiyonuai unatekelezwa. Kazi hiyo imefanywa na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine - SUA, na sasa utafiti huo umekamilika, Je umebaini nini? John Kabambala wa redio washirika KidsTime ya Morogoro-Tanzania amehudhuria uzinduzi wa ripoti hiyo ya vipimo vya udongo.

Ripoti hiyo ya mpango wa upimaji udongo imewasilishwa mbele ya wadau kutoka  sekta za Kilimo na uhifadhi wa Mazingira.