Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO inavyofungua uwezo: Simulizi ya kijana mkimbizi Gad Harindimana Mnyarwanda nchini Uganda

Gad Harindimana, kijana mkimbizi kutoka Rwanda anayeishi katika makazi ya wakimbizi ya Nakivale nchini Uganda.
ILO
Gad Harindimana, kijana mkimbizi kutoka Rwanda anayeishi katika makazi ya wakimbizi ya Nakivale nchini Uganda.

FAO inavyofungua uwezo: Simulizi ya kijana mkimbizi Gad Harindimana Mnyarwanda nchini Uganda

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Gad Harindimana, kijana mkimbizi kutoka Rwanda anayeishi katika makazi ya wakimbizi ya Nakivale amepata kazi ya ufundi pikipiki baada ya kukamilisha programu ya Huduma za Ajira Vijijini inayoungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi Duniani, ILO na shirika lisilo la kiserikali la AVSI Foundation.

Mpango huu wa kibunifu unaoungwa mkono na ILO unatoa huduma maalum za ajira zinazofaa kwa mazingira ya maeneo husika, unaongeza uwezo wa kuajiriwa wa wakimbizi na jamii zinazowakaribisha kupitia huduma za kuoanisha kazi, hutoa usaidizi wa kutafuta kazi na ushauri, hutoa taarifa za soko la ajira na mapendekezo kwa sera za soko la ajira.

Soundcloud

Harindimana anasimulia hatua kwa hatua safari ya mafanikio yake

Tuliondoka Rwanda kutokana na matatizo yaliyotokea tukahamia Bunyoro. Tulipofika Bunyoro shida zikazidi wakaniambia nina shangazi huku ndipo nikahamia huku kwenye kambi ya wakimbizi na nikapata cheti. 

Majina yangu ni Gad Harindimana, mimi ni Mnyarwanda. Nilipokuwa bado ninaisho Hoima nilikuwa sijawahi kwenda shule. Nilipofika huku ndipo nikaingia shule. Nilipofika humu kwenye makazi ya wakimbizi Nakivale shangazi yangu akanianzisha shule nikaanza kusoma darasa la kwanza. Nilipofika darasa la nne, ada ya shule ikakosekana nikabaki nyumbani. 

Hapo nikaanza kujituma kuteka maji na kulima ili kujipatia kipato. 

Siku moja nilipokuwa ninateka maji nikasikia kuhusu AVSI Foundation wanasajili vijana ambao wanawasaidia kuwasomesha ufundi, kinyozi na vingine vingi walikuwa wanasaidia kwa namna nyingi. Nikajisikia mimi napenda umakenika. Nikaja nikawauliza, wakanitaka cheti nikakileta wakaniandika. Nikarudi nyumbani nikamuuliza shangazi akasema ni sawa.

Watu wa AVSI walipomaliza kutusajili wakatupeleka gereji wakasema watakuwa wanatulipa kupitia ufadhili wa ILO. Wakatuleta wakatukabidhi kwa mkufunzi. Alikuwa anaitwa Salongo. Tukaanza kusoma kwa miezi sita. Tukajifunza namna ya kurekebisha tairi, pistoni, vitu kama kuziba pancha. Tulijifunzia kwenye pikipiki. 

Kilichonihamasisha kuingia katika umakenika nilifikiria kwa mfano nikitoka hapa nikafika Rwanda au popote ninaweza kufanya kazi kwa kuwa nimeisome kazi hii.

Baada ya miezi sita ya kusoma tulifanya mtihani. Baadaye wakatueleza matokeo na watu wa gereji wakaona matokeo ni mazuri wakaniambia nibaki. Wakanipa kazi nikafurahi sana. Nikajua sasa angalau nitakuwa ninapata ka pesa kiasi. 

Gad Harindimana, kijana mkimbizi kutoka Rwanda anayeishi katika makazi ya wakimbizi ya Nakivale nchini Uganda, akiwa na mjasiriamali mwenzake.
ILO
Gad Harindimana, kijana mkimbizi kutoka Rwanda anayeishi katika makazi ya wakimbizi ya Nakivale nchini Uganda, akiwa na mjasiriamali mwenzake.

Sasa hivi ninaweza nikatengeneza pikipiki nikapata dola 5 au mbili. Kwaweli mambo sasa hivi yamebadilika kiasi na nafurahi sana kupata kazi. 

Ninawashukuru AVSI na ILO ambao walitufadhili kwa kuwa wanakuwa wanatufuatilia na kuangalia tunavyoendelea. Wametusomesha ninaweza kutumia mikono yangu kujikimu. 

Sasa ninawashukuru sana na kuwaomba waendelee kuwasaidia vijana wenginge kama sisi kwa kuwa wengi bado wanahangaika.