Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tutafanikisha suala la bima na kufikia afya kwa wote Tanzania 2030: Ummy Mwalimu

Waziri wa afya wa Tanzania Ummy Mwalimu akiwa mkutanoni kwenye Baraza Kuu ya Umoja wa Mataifa.
UN News
Waziri wa afya wa Tanzania Ummy Mwalimu akiwa mkutanoni kwenye Baraza Kuu ya Umoja wa Mataifa.

Tutafanikisha suala la bima na kufikia afya kwa wote Tanzania 2030: Ummy Mwalimu

Afya

Waziri wa afya wa Tanzania Ummy mwalimu amesema ana imani kubwa kwamba Tanzania iko mbioni kutimiza lengo la Umoja wa Mataifa la afya kwa wote ifikapo mwaka 2030.

Akizungumza na idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa mwishoni mwa juma baada ya kupitishwa azimio la kuchukua hatua kusu utekelezaji wa afya kwa wote waziri Ummy amesema Tuna rasilimali watu, tuna miundombinu na tuna fedha kinachotukwamisha ni bima ya afya kwa wote ili kutimiza lengo na azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu huduma za afya kwa wote ifikapo mwaka 2030.”

Amesema taifa hilo la Afrika Mashariki linafanya kila jitihada kuweza kufikia lengo hilo na hata kabla ya kupitishwa kwa azimio  amnbalo inaliunga mkono tayari ilikuwa imeanza kuchukua hatua endelevu za kuhakikisha kila Mtanzania popote alipo anapata huduma bora na bila vikwazo vyovyote.

Kinachofanyika kufikia lengo

Waziti Ummy amesema kubwa ambalo tumelifanya kwanza “ni kuongeza miundo mbinu ya kutoa huduma za afya, kwa hiyo tumejenga sana zahanati katika ngazi ya vijiji, vituo vya afya katika ngazi ya kata, hospital za halimashauri , hospital za rufaa za mikoa, hospital za Kanda pamoja na hospital za kitaifa.

Ameongeza kuwa pia wataendelea kusogeza huduma za afya karibu na wanchi kwa kujenga miuondombinu inayohitajika na kuhakikisha vitaa muhimu vinapatikana.

Pili amesema “Ni kuhakikisha tunaongeza na kuimarisha huduma za uchunguzi hususan kununua vifaa tiba vya kisasa.

Tatu ni “ Kuongeza rasilimali watu au watumishi wa afya kwani kwa sasa hatuna shida sana katika wahudumu wa afya ila tunachangamoto katika hawa madaktari bingwa wa kutosha kutoa huduma za afya.

Amesisitiza kuwa hilo linafanyiwa kazi na litapatiwa ufunzi ikiwemo kuchagiza mafunzo zaidi kwa wahudumu wa afya.

 

 Changamoto ya kutokuwa na bima ya afya

Waziri Ummy amesema changamoto kubwa inayolikabili taifa hilo ikitatuliwa itaisaidia Tanzania kutimiza leo la huduma ya afya kwa wote na changamoto hiyo ni gharama za huduma na watu kutokuwa na bima kwani

“ Asilimia 85 ya Watanzania wanapata huduma za afya kwa kulipia fedha taslimu na hiyo ndio changamoto kubwa na inawafanya Watanzania wanaingia katika umasikini zaidi kwa mfano tumepata kesi mtu anauza kipande cha shamba, anauza nyumba yake, anauza baiskeli yake pale anapokuwa mgonjwa au  anapouguza mpendwa wake..”

Waziri wa afya wa Tanzania Ummy Mwalimu.
UN News
Waziri wa afya wa Tanzania Ummy Mwalimu.

Je serikali inafanya nini sasa kushughulikia changamoto hiyo

Ummy amesema sasa ili kufikia huduma ya afya kwa wote “ Ni kuhakikisha tunaingiza Watanzania wengi katika mfumo wa bima ya afya , na ndio maana kama serikali tumeshawasilisha bungeni mswaada wa sheria ya bima ya afya kwa wote kuwawezesha Watanzania kupata huduma za afya bila kikwzo cha fedha.

Ameongeza kuwa na bima hiyo kwa kuwa itakuwa ni ya umma watahakikisha ni ya gharama nafuu kila Mtanzania ataweza kumudu.

Pili amesema kwa kuwa Watanzania wengi hawawezi kumudu kulipia gharama kwa mara moja wanafikiria kuja na mbinu mbalimbali zitakazowawezesha wananchi kulipia bima hiyo kwa kudunduliza.

Tatu serikali itahakikisha wananchi wanapata huduma boraa ambazo ni salama na kwa wakati.

Kwa mantiki hiyo waziri Ummy amesema wakitekeleza hayo basi anaamini Tanzania itafikia lengo la kuhakikisha huduma za afya kwa wote ifikapo mwaka 2030.