Ripoti ya SOFI: Watu milioni 122 wanakabiliwa na njaa duniani
Zaidi ya watu milioni 122 wanakabiliwa na njaa duniani tangu mwaka 2019 kutokana na majanga mbalimbali, mishtuko ya hali ya hewa pamoja na migogoro ya mara kwa mara ikiwa ni pamoja na vita vya Ukraine hayo yapo kwenye ripoti iliyotolewa leo ya hali ya usalama wa chakula na lishe duniani SOFI.