Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WMO: Ulimwenguni kulikuwa na kiwango cha juu cha joto

Viwango vya joto vya uso wa bahari vilifikia rekodi ya juu zaidi Mei na Juni 2023.
Unsplash/Rafael Garcin
Viwango vya joto vya uso wa bahari vilifikia rekodi ya juu zaidi Mei na Juni 2023.

WMO: Ulimwenguni kulikuwa na kiwango cha juu cha joto

Tabianchi na mazingira

Ulimwengu ulikuwa na siku chache za joto kiwango cha juu zaidi kwenye rekodi, kulingana na takwimu za awali zilizotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa WMO.

Taarifa ya shirika hilo imesema kiwango hicho kinafuata hali iliyorekodiwa mwezi Juni ambao ulirekodi halijoto isiyo na kifani kwenye uso wa bahari na rekodi ya kiwango cha chini cha barafu katika bahari ya Antaktika. 

Mkuu wa ufuatiliaji wa hali ya hewa wa WMO Dkt. Omar Baddour amesema takwimu mbalimbali za uchambuzi upya zinazozalishwa na vituo tofauti ulimwenguni zimeonesha kuendana. 

“Hata hivyo ni mapema kutathmini kile ambacho kinawakilisha katika suala la viwango vya joto vya kila siku vya dunia kwenye ardhi kulingana na uchunguzi halisi ambao unahitaji mchakato mkali wa udhibiti wa ubora, kama WMO inavyofanya kwenye utoaji wa taarifa zake za hali ya kimataifa ya hewa.” 

Kwa mujibu wa uchambuzi wa takwimu za muda uliofanywa na Wakala wa Hali ya Hewa wa Japan, wastani wa halijoto duniani tarehe 7 Julai ilikuwa nyuzi joto 17.24. Hii ni Selsiasi 0.3° juu ya rekodi ya awali ya Selsiasi 16.94(°C) mnamo tarehe 16 Agosti 2016 ambao ulikuwa ni mwaka wa El Niño wenye nguvu.

Hata hivyo takwimu hizo za uchambuzi wa Kijapani bado haijathibitishwa. Lakini inalingana na takwimu za awali kutoka kwa hifadhidata ya Copernicus ECMWF ERA5.

Dkt. Baddour amesema hata hivyo, rekodi hizi za muda zinatoa ushahidi mwingine wa mabadiliko ya tabianchi duniani kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na kipindi cha El Niño.

Hali hii inamaanisha nini? 

Viwango vya joto vinavyovunja rekodi kwenye nchi kavu na baharini vina athari zinazoweza kuathiri mifumo ya ikolojia na mazingira. Viwango hivyo vinaonesha mabadiliko makubwa yanayotokea katika mfumo wa dunia kama hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi hazitachukuliwa, athari zinazo sababishwa na mwanadamu.

Mwishoni mwa Mwezi Juni 2023 WMO ilitangaza kutakuwa na tukio la El Niño mwaka huu, na kwa taarifa hii ya leo inaonesha tukio hilo sasa liko katika hatua za mwanzo, linatarajiwa kuongeza joto zaidi ardhini na baharini, na kusababisha halijoto kali zaidi na mawimbi ya joto baharini.

Viwango vya joto mwezi Juni

Mwezi Juni ulikuwa na hali ya ukavu kuliko wastani katika sehemu kubwa ya Amerika kaskazini, hali ambayo iliendeleza moto mkali wa nyikani.

Pembe ya Afrika na sehemu kubwa ya kusini mwa bara la Afrika kulikuwa na hali ya ukame, sawa na hali ilivyokuwa katika nchi ya Urusi, Amerika Kusini, na maeneo ya Australia, kulingana na taarifa iliyotolewa na Huduma ya Mabadiliko ya Tabianchi ya Copernicus.

Viwango vya juu vya joto kwa mwezi Juni vilirekodiwa kote kaskazini-magharibi mwa bara la Ulaya, kulingana na Copernicus. Sehemu za nchi za Canada, Marekani, Mexico, Asia, na Australia mashariki zilikuwa na joto zaidi kuliko kawaida.

Hata hivyo hali ilikuwa baridi kuliko kawaida huko magharibi mwa Australia, Magharini mwa Marekani, na Magharibi wanchi ya Urusi.

Kusoma zaidi kuhusu taarifa hii bofya hapa.