Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutopitishwa azimio la Baraza la Usalama ni hatari kwa Wasyria 

Baba na mwanae wakiwa wamebeba hema la familia kwenye kambi ya Kerama huko Kaskazini mwa Syria karibu na eneo la Bab Al-Hawa mpakani na Uturuki.(Maktaba)
UNHCR
Baba na mwanae wakiwa wamebeba hema la familia kwenye kambi ya Kerama huko Kaskazini mwa Syria karibu na eneo la Bab Al-Hawa mpakani na Uturuki.(Maktaba)

Kutopitishwa azimio la Baraza la Usalama ni hatari kwa Wasyria 

Msaada wa Kibinadamu

Baada ya jana Jumanne nia ya Baraza la Usalama kupitisha azimio ambalo ningeruhusu uvushaji misaada ya kibinadamu katika kivuko cha Bab al-Hawa kwenye mpaka wa Syria na Uturuki kaskazini-magharibi mwa Syria ili ikaokoe maisha ya wananchi wa nchi hiyo ambao wamekuwa kwenye zaidi ya miaka 12 ya vita kukwama kutokana na Urusi kupiga kura ya turufu kulipinga azimio hilo lingerefusha operesheni hiyo kwa miezi tisa mbele baada ya kufikia ukomo juzi tarehe 10 Julai, hofu sasa ni kuwa matokeo yake yatakuwa maumivu zaidi kwa wananchi wa Syria. 

Huyo ni Priscilla Gomes mmoja wa maafisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR akiwa huko kaskazini-magharibi mwa Syria anasema…kwa sasa yuko Atma, katika moja ya vituo vya jamii vinavyoungwa mkono na UNHCR

Priscilla Akieleza umuhimu wa misaada ya kibinadamu huko anasema,  "Hapa, watoto na watu wazima ambao wameathiriwa na migogoro na tetemeko la ardhi wanaweza kupata huduma muhimu za ulinzi, ikiwa ni pamoja na ushauri wa kisheria, msaada wa kisaikolojia, na upatikanaji wa shughuli za jamii na mafunzo ya ufundi.” 

Takribani watu milioni 4.1, ambapo inakadiriwa milioni 2.7 ni wakimbizi wa ndani, wanaendelea kuhitaji msaada muhimu wa kuokoa maisha.  

Wakati Umoja wa Mataifa na wadau wake wametayarisha mpango wa mwendelezo wa utoaji misaada, pengo lililoletwa na kutopitishwa mwendelezo wa azimio la kuvusha misaada kutoka Türkiye hadi kaskazini-magharibi mwa Syria kunaweza kuongeza mateso ya wanadamu kwa haraka. 

Priscilla Gomes afisa huyu wa UNHCR akiwa bado kaskazini magharibi mwa Syria anahitimisha akisema, "Ni muhimu kutoa msaada wa haraka wa kuokoa maisha. Na ni muhimu pia kuunga mkono mwitikio katika muda wa kati na mrefu, kushughulikia mahitaji makubwa.