Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katikati ya mchakato: Njia 5 zinazotumiwa na UN kuharakisha ufikiaji wa SDGs

Zara Bulama akiwa amebeba mmoja wa mbuzi wake aliopokea kutoka FAO katika eneo la Gongulong, Maiduguri, Nigeria, mwezi Juni 2021.
UNOCHA/Damilola Onafuwa
Zara Bulama akiwa amebeba mmoja wa mbuzi wake aliopokea kutoka FAO katika eneo la Gongulong, Maiduguri, Nigeria, mwezi Juni 2021.

Katikati ya mchakato: Njia 5 zinazotumiwa na UN kuharakisha ufikiaji wa SDGs

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Katika nusu ya mchakato wa hatua za kufikia ajenda kabambe ya 2030 ya Maendeleo Endelevu, nchi wanachama, wavumbuzi, na washawishi wamekusanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa leo Jumatatu wakati Baraza la uchumi na kijamii la Umoja wa Mataifa (ECOSOC) litakuwa linaonyesha mafanikio yaliypopatikana baada ya janga la COVID-19 katika harakati za kuelekea utimizaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), likizindua ripoti yake ya hivi karibuni ya maendeleo.

Hapa kuna mambo matano muhimu unayohitaji kuyajua:

1) Kurejea kwenye mstari

Janga la coronavirus">COVID-19 lilirejesha nyuma mafanikio yaliyopatikana katika kufikia SDGs kwa miongo kadhaa, na, ikiwa hali ya sasa itaendelea, ifikapo 2030, watu milioni 575 wataendelea kubaki kwenye umaskini uliokithiri, kulingana na ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa.

Wastani wa halijoto duniani tayari umepanda karibu nyuzi joto 1.1°C juu ya viwango vya kabla ya mapinduzi ya viwanda na kuna uwezekano wa kufikia au kuvuka kiwango muhimu cha nyuzi joto 1.5°C kufikia mwaka 2035.

Kinachoongoza njia ya kusaidia mataifa kurejea kwenye mstari ni jukwaa la kisiasa la ngazi ya juu la Baraza  la kiuchumi na kijamii ECOSOC (HLPF) lililoanza leo Jumatatu.

Jukwaa hilo limewaleta pamoja nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, pamoja na mashirika ya kiraia, viongozi wa sekta na wabunifu, na watakutana hadi tarehe 20 Julai, na kutathimini malengo matano kati ya 17 ya SDGs, na kazi yao kuelekea katika mkutano muhimu wa SDG uanaotarajiwa kufanyika mwezi Septemba mwaka huu.

"Maendeleo ya malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs) yamekwama kwa kiasi kikubwa. Kuashiria tuko katikati ya ukomo wa malengo hayo tunatumai tunaweza kuhamasisha umakini." rais wa ECOSOC Lachezara Stoeva amewaambia waandishi wa habari siku ya Ijumaa.

Chini ya mada ya kuongeza kasi ya kujikwamua baada ya COVID-19, karibu nchi 40 zitawasilisha hadithi za mafanikio pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo kuelekea kufikia malengo, na zaidi ya mawaziri 100 pamoja na mashirika ya kiraia, wanazuoni na wabunifu kutoka kote ulimwenguni wataeleza waliojifunza na safu ya suluhu za kibunifu ili kusaidia kufikia mstari wa kumalizia utimizaji wa malengo hayo.

2) Kuongeza kasi ya upatikanaji wa maji safi, usafi wa mazingira, na nishati

Sukhdev Vishwakarma na binti yake Meenu wote wakiwa ni wakulima wanatu,mia maji ya kisima cha kupampu na sola katika shamba la Gurinder Singh lenye ukubwa wa ekari 80 Jagadhri.
© CCAFS/Prashanth Vishwanathan
Sukhdev Vishwakarma na binti yake Meenu wote wakiwa ni wakulima wanatu,mia maji ya kisima cha kupampu na sola katika shamba la Gurinder Singh lenye ukubwa wa ekari 80 Jagadhri.

Takriban watu bilioni mbili bado wanaishi bila huduma za maji ya kunywa zinazosimamiwa kwa usalama, jambo linaloleta changamoto kubwa katika kutimiza lengo la SDG 6.

Kadhalika, wakati idadi ya watu wasio na umeme ilipungua kutoka bilioni 1.2 hadi milioni 733 kati ya mwaka 2010 na 2020, ufuatiliaji wa SDG 7, ripoti ya maendeleo ya nishati ilionya kuwa juhudi za sasa hazitoshi kufikia lengo kwa wakati.

Sehemu ya tatizo ni fedha. Ili kufikia malengo haya, kushirikisha sekta kibinafsi na washirika wengine wapya kutakuwa muhimu katika kufungua uwekezaji mpya.

Nyakati tayari zinabadilika. Nishati inayojali mazingira sasa inaonekana kama sekta ya ukuaji ambayo inaweza kuunda ajira na kuongeza ustawi. 

Mwaka 2022, kwa mara ya kwanza, uwekezaji katika nishati ya safi ulizidi ule wa nishati ya kisukuku, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

HLPF itasikia kutoka kwa mataifa kama Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), ambayo yanaingia kwenye mabadiliko kwa msaada kutoka kwa washirika wanaoendelea. 

Kwa kufunga mashamba mapya ya nishati ya jua au sola na kukarabati kituo cha kuzalisha umeme cha Boali, Serikali ya CAR iliongeza upatikanaji wa umeme katika miji kutoka asilimia 14.3 hadi asilimia 32 kati ya mwaka 2018 na 2022.

  1. Reaping benefits, from robots to resilience
AfriLeap inazalisha na kusambaza hope cones zenye ubora wa hali ya juu na hivyo kuwawezesha wakulima, kuokoa ardhi na maji
© AfriLeap
AfriLeap inazalisha na kusambaza hope cones zenye ubora wa hali ya juu na hivyo kuwawezesha wakulima, kuokoa ardhi na maji

Wakati janga la COVID-19 liliathiri karibu kazi moja kati ya tatu katika tasnia ya utengenezaji na uzalishaji , sekta ya uwekezaji wa uvumbuzi ulibaki thabiti kadiri bajeti za za utafiti na maendeleo za mashirika na serikali zilivyokua, kulingana na Umoja wa Mataifa. 

Ongezeko kubwa zaidi lilikuwa katika suala la mtaji, ambao umekuwa ukifanya kazi sana barani Afrika, Amerika Kusini, na Karibea.

Kuanzia kutumia faida za roboti hadi uwezo wa washawishi kama Jane Goodall, Ciara, na Yo-Yo Ma katika mtandao wake wa wafuasi duniani kote, Umoja wa Mataifa na washirika wanasaidia mipango mbalimbali ya kuangazia kazi inayofanywa kusaidia mataifa kuendesha ukuaji unaojali mazingira katika sekta zote kufikia lengo la SDG 9, kwenye tasnia ya uvumbuzi na miundombinu.

Katika muda wote wa kongamano hilo, ushirikiano wa sayansi, teknolojia na uvumbuzi utaangaziwa, pamoja na zaidi ya mikutano 200 ya kando ili kuonyesha suluhu mbalimbali za ubunifu na kuendeleza malengo.

Mfano wa kinachotolewa ni pamoja na kuzinduliwa kwa muhtasari wa sera ya Umoja wa Mataifa ya Nishati, Ramani ya Kimataifa ya harakati za kuelekea  kwenye haki ya nishati safi ya kupika na Jumuishi, na tukio la Mameya la Go Digital, ambalo linakuza muungano wa kimataifa wa mameya kwa ushirikiano wa kidijitali ili kutumia teknolojia hizi kwa maendeleo endelevu na shirikishi ya mijini.

Luanda, Angola.
© UNDP Angola/Cynthia R Matonho
Luanda, Angola.

4) Miji ya kijani kwa wote

Miji itakuwa viwanja muhimu vya vita katika mjchakato wa kufikia ajenda ya 2030, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alisema mwezi Juni. Ikizalisha asilimia 70 ya gesi chafuzi duniani na makazi ya nusu ya binadamu wote, miji iko mstari wa mbele kuchukua hatua huku mataifa yakijitahidi kuweka mazingira ya miji kuwa ya kijani yanayojali mazingira.

Katika muda wa miaka 30, makadirio ya Umoja wa Mataifa yanaonyesha kwamba zaidi ya theluthi mbili ya watu watapendelea kuishi katika miji mikubwa na majiji, wakivutiwa na faida zilizopo. 

Katika vichochezi muhimu vya ukuaji wa uchumi, miji inachangia zaidi ya asilimia 80 ya pato la taifa.

Lakini, mwaka wa 2020, zaidi ya watu bilioni moja waliishi katika makazi duni au makazi yasiyokuwa rasmi, wengi wao katika bara Asia na Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kadiri idadi ya watu wa mijini inavyoongezeka, makazi duni huongezeka kwa kasi zaidi.

SDG 11 inalenga kushughulikia masuala haya kwa kufanya miji na makazi ya watu kuwa shirikishi, salama, thabiti na endelevu ifikapo mwaka 2030. 

Hiyo ina maana kutafuta suluhu, ambazo kongamano hili litajadili.

“Hii ni pamoja na kubadilisha makazi duni na makazi yaliyopitwa na wakati na kuwa na makazi yanayofaa, kuanzisha mifumo ya usafiri wa gharama nafuu na wa kutegemewa, na kuhakikisha upatikanaji wa huduma muhimu sambamba na kuunda mazingira ya mijini yenye maeneo ya kijani kibichi yanayofikiwa na wote.”

Mwanasayansi nchini Venezuela akitafiti usugu wa vijiuavijasumu (AMR) ambao ni moja ya hatari 10 zinazoikabili dunia katika suala la afya
© WHO/Sarah Pabst
Mwanasayansi nchini Venezuela akitafiti usugu wa vijiuavijasumu (AMR) ambao ni moja ya hatari 10 zinazoikabili dunia katika suala la afya

5) Ushirikiano wa ubunifu

SDGs zinaweza kufikiwa tu kupitia ushirikiano thabiti, rais wa ECOSOC alisema Ijumaa. 

Ndiyo maana HLPF itakuwa inasikiliza kutoka kwa wawakilishi wa mashirika ya kiraia, sekta kibinafsi, na wanazuoni.

Sehemu ya changamoto ni ufadhili, alisema, na kuongeza kuwa "tunahitaji kujumuisha sekta binafsi na kuangalia njia mpya za kufadhili malengo."

Washirika wapya pia wanahitajika, aliongeza akibainisha kuwa vyombo vya habari vinaweza kuchukua jukumu kubwa katika kukuza juhudi zinazoendelea. Ikionyesha hali ya kuunganishwa kwa malengo yote, SDG 17 pia inataka ushirikiano katika na kufikia sayansi, teknolojia na uvumbuzi, kwaaina fiulani, ili kuhakikisha kwamba mataifa yote yanaweza kufaidika kutokana na maendeleo mapya.

Kupitia kongamano hilo, nchi na washikadau wakuu watabadilishana uzoefu na manufaa kutokana na ushirikiano katika kukabiliana kwa pamoja na baadhi ya changamoto kubwa zaidi za maendeleo endelevu, katika jitihada za kuendeleza maendeleo kuelekea kufikia SDGs na bila kumwacha mtu yeyote nyuma.

Msichana akiwasiliana na roboti mjini Osaka Japan
© Unsplash/Andy Kelly
Msichana akiwasiliana na roboti mjini Osaka Japan