ICC yaanzisha uchunguzi dhidi ya kuongezeka kwa ghasia Darfur Sudan
Mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC amesema leo kwamba anachunguza madai mapya ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu katika jimbo la Darfur nchini Siudan, ikiwa ni pamoja na mauaji ya hivi karibuni ya watu 87 wa jamii ya kabila la Masalit, yaliyoripotiwa kutekelezwa na vikosi vya msaada wa haraka RSF Rapid na wanamgambo wake.