Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICC yaanzisha uchunguzi dhidi ya kuongezeka kwa ghasia Darfur Sudan

Wanawake kutoka nchini Sudan wakitembea mahali salama Um Baru, Kaskazini mwa Darfur (Kutoka Maktaba).
UNAMID/Hamid Abdulsalam
Wanawake kutoka nchini Sudan wakitembea mahali salama Um Baru, Kaskazini mwa Darfur (Kutoka Maktaba).

ICC yaanzisha uchunguzi dhidi ya kuongezeka kwa ghasia Darfur Sudan

Amani na Usalama

Mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC amesema leo  kwamba anachunguza madai mapya ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu katika jimbo la Darfur nchini Siudan, ikiwa ni pamoja na mauaji ya hivi karibuni ya watu 87 wa jamii ya kabila la Masalit, yaliyoripotiwa kutekelezwa na vikosi vya msaada wa haraka RSF Rapid na wanamgambo wake.

Akitoa taarifa hiyo kwa Baraza la Usalama la U,moja wa Mataifa , mwendesha mashtaka huyo Karim Khan, amesema mamlaka ya ofisi yake, kwa mujibu wa azimio nambari 1593 kuhusu hali ya Darfur iliyowasilishwa kwenye mahakama hiyo mwaka 2005, iliweka bayana kwamba

“Jukumu letu linaendelea kuhusiana na uhalifu ndani ya mamlaka yetu, uhalifu wa mauaji ya kimbari, uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita na mtu yeyote atakayebainika kufanya uhalifu huo ndani ya mamlaka yetu atachunguzwa.” 

Hakuna kitakachofumbiwa jicho

"Na kulingana na tathmini za majaji huru wa ICC, tutachuja kila mshipa na kutoacha jambo lolote ili kuhakikisha kwamba wanawajibishwa katika kesi kwa haki na huru."

Bwana Khan ameendelea kulitaka Baraza la Usalama la wanachama 15 "kukutana kwa muktada wa kanuni za mkataba wa Umoja wa Mataifa, majukumu chini ya mkataba wa Roma wa ICC, na mamlaka ya Baraza lenyewe, ambalo mmwaka 2005 liliamua kwamba ghasia katika eneo la Darfur na Sudan kwa ujumla, ziliwakilisha tishio kwa amani na usalama wa kimataifa."

Mwendesha Mashtaka huyo amesisitiza kwamba "Na haitumiki tu katika vitendo vilivyofanywa nchini Sudan, mtu yeyote ambaye anasaidia, kushawishi, kuhimiza au kuelekeza kutoka nje ya Sudan uhalifu unaoweza kufanywa huko Darfur pia atachunguzwa." 

Hakuna kitakachofumbiwa jicho

"Na kulingana na tathmini za majaji huru wa ICC, tutachuja kila mshipa na kuacha jambo lolote kuhakikisha kwamba wanawajibishwa katika kesi za haki na huru."

Bwana Khan ameendelea kulitaka Baraza la Usalama la wanachama 15 kukutana kwa muktabda wa kuzunguka kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa, majukumu chini ya Mkataba wa Roma wa ICC, na mamlaka ya Baraza lenyewe, ambalo mwaka 2005 liliamua kwamba ghasia katika eneo la Darfur na Sudan kwa ujumla, iliwakilisha tishio kwa amani na usalama wa kimataifa.

"Na halitumiki tu katika vitendo vilivyofanywa nchini Sudan, mtu yeyote ambaye anasaidia, kushawishi, kuhimiza au kuelekeza uhalifu kutoka nje ya Sudan unaoweza kufanywa huko Darfur pia atachunguzwa," mwendesha mashtaka amesisitiza.

Maelekezo yaliyo wazi

Bwana Khan amewafahamisha mabalozi kwamba ametoa "maelekezo ya wazi kwa ofisi yake kuweka kipaumbele kwa uhalifu dhidi ya watoto, na uhalifu wa unyanyasaji wa kijinsia na kingono.”

Pia ametangaza kuwa tovuti salama ya mtandaoni imeanzishwa ambapo watu binafsi wanaweza kuwasilisha taarifa au madai ya uhalifu na ukiukaji wa haki za binadamu.

"Tutahakikisha, Mungu akipenda, kwamba haki haizungumzwi tu katika chumba hiki cha Baraza la Usalama, lakini inahisiwa kutetea haki za raia na walio hatarini kwa njia ambazo hawajaona vya kutosha katika uzoefu wao wa maisha," Amesema Bwana Khan.

Kulinda sheria za kimataifa

Mwendesha mashtaka huyo wa ICC pia ametoa wito kwa pande zinazozozana nchini Sudan kuzingatia wajibu wao wa msingi chini ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu na kuwalinda raia.

"Ni muhimu kwamba wale wanaohusika katika uhasama watambue hata kama ni muda gani wa siku wanapaswa kuzingatia wajibu wao chini ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu," amesisitiza.

Karim Khan mwendesha mashitaka wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC
UN Photo/Manuel Elías
Karim Khan mwendesha mashitaka wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC

 

Taarifa kuhusu kesi

Katika taarifa yake Bwa Khan pia ametoa maelezo kwa mujibu wa azimio namba 1593, ikiwa ni pamoja na maendeleo katika kesi ya Ali Muhammad Ali Abd-Al-Rahman, kiongozi mkuu wa wanamgambo wa Janjaweed huko Darfur, pamoja na kesi zingine zikiwemo za rais  wa zamani Omar Al Bashir, na mawaziri wa zamani Ahmad Muhammad Harun na Abdel Raheem Muhammed Hussein, ambao wanashitakiwa kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

"Kuongezeka kwa hali ya uhasama mkubwa, ikiwa ni pamoja na madai ya uhalifu, na hali ya sasa ya taasisi za Sudan, inadhihirisha zaidi kutoweza kwa Serikali ya Sudan kutoa kipaumbele kwa haki na uwajibikaji," imesema ripoti hiyo.

"Katika hali ya sasa, haiwezekani kushiriki katika majadiliano na serikali ya Sudan kuhusu kukamilishana," imeongeza, ikibainisha kuwa ofisi ya mwendesha mashtaka inashirikiana na washirika husika kuhusu hati za kukamatwa ambazo hazijakamilika dhidi ya Bwana Al Bashir, Bwana Hussein na Bwana Harun, hasa kwa kuzingatia uhasama unaoendelea kati ya jeshi la taifa na wanamgambo wa RSF.