UNODC na UNESCO zajengea vijana uwezo kuwa wajenzi wa amani
Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kukabili madawa ya kulevya na uhalifu Ghada Waly amesema pamoja na kufanya tafiti za kuelewa vema uhusiano kati ya uhalifu wa kupangwa na ugaidi Afrika ni muhimu pia kuwa na sera na miradi ya kukabili vitendo hivyo haramu.