Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Bi. Krishnakumar Jeyaranjini, mnufaika wa mradi wa ILO wa kujengea uwezo wa kiuchumi kaya zinazoongozwa na wanawake nchini Sri Lanka hasa maeneo yaliyokuwa yameathiriwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
ILO

Mradi wa ILO waleta matumaini kwa watamil nchini Sri Lanka

Nchini Sri Lanka, serikali na mradi wa pamoja wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya amani kupitia shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO, wanatekeleza mradi wa kuinua jamii za watamil ambazo zimerejea kwenye makazi yao baada ya mzozo wa muda mrefu kaskazini mwa nchi hiyo, mradi ambao unawezesha jamii kujumuika tena na kushiriki kwenye shughuli za kiuchumi na kuinua kipato chao baada ya mzozo uliodumu kwa takribani miaka 25.

Sauti
2'3"
Mwanamke akiwa amepiga picha mbele ya mchoro unaowakilisha jua wakati wa siku ya afya ya akili duniani
UN Photo: M. Perret

Ni wakati wa kuhakikisha afya ya akili kwa wote ni kipaumbele cha kimataifa:Guterres 

Wakati umefika wa kuhakikisha afya ya akili kwa wote inakuwa ni kipeumbele cha kimataifa amesema hii leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akikisitiza kwamba hicho ni kipaumbele chake katika Umoja wa Mataifa na anafahamu kuwa ni changamoto kubwa kote duniani kushughulikia suala la afya ya akili. Flora Nducha na taarifa kamili 

Sauti
2'10"
Ndege wahamiaji wakiwa katika safari zao kuelekea kusini.
Picha ya WMB

Leo ni siku ya Ndege wanaohama duniani 

Oktoba 8 kila mwaka ni siku ya Ndege wanaohama duniani. Mwaka huu siku hiyi imejikita katika katika tatizo la mwanga wa bandia wa taa ambayo unaleta tishio kubwa kwa ndege, kwani unaongoza kwa kuchanganyikiwa kwao wakati wa usiku ndege hao wanaposafiri na kuharibu mwelekeo wao  wakati wanapohama kwenda umbali mrefu.

Watu waliofurushwa nchini Burkina Faso wakiwa kambini mjini Pissila kasakazini mashariki mwa nchi hiyo.
WFP/Marwa Awad

Tunafuatilia kwa karibu hali ya haki za binadamu nchini Burkina Faso – Ofisi ya Haki za Binadamu UN 

Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR kupitia Msemaji wake Seif Magango akiwa jijini Nairobi, Kenya leo Ijumaa amesema wanakaribisha taarifa za mamlaka za kijeshi kwamba zitaheshimu "ahadi za kimataifa za nchi, ikiwa ni pamoja na zile zinazohusiana na kukuza na kulinda haki za binadamu,” lakini wanasalia na wasiwasi kwamba madai mengi ya ukiukaji wa haki za binadamu yanaendelea kuripotiwa kutoka sehemu nyingi za nchi. 

Ales Bialiatski wa pili kushoto wakati wa hafla ya tuzo ya Wlodkowic kenye bunge la Poland mwaka 2014
© Michał Józefaciuk

Washindi wa tuzo ya amani ya Nobel 2022 watangazwa 

Kamati ya tuzo ya amani ya Nobel ya Norway leo imetangaza washini wa tuzo ya amani ya Nobel kwa mwaka 2022 kuwa ni "Mtetezi wa haki za binadamu Ales Bialiatski kutoka Belarus, shirika la haki za binadamu la Urusi Memorial na shirika la haki za binadamu la Ukraine Center for Civil Liberties ambao wanawakilisha jumuiya za kiraia katika nchi zao.”