Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo ni siku ya Ndege wanaohama duniani 

Ndege wahamiaji wakiwa katika safari zao kuelekea kusini.
Picha ya WMB
Ndege wahamiaji wakiwa katika safari zao kuelekea kusini.

Leo ni siku ya Ndege wanaohama duniani 

Masuala ya UM

Oktoba 8 kila mwaka ni siku ya Ndege wanaohama duniani. Mwaka huu siku hiyi imejikita katika katika tatizo la mwanga wa bandia wa taa ambayo unaleta tishio kubwa kwa ndege, kwani unaongoza kwa kuchanganyikiwa kwao wakati wa usiku ndege hao wanaposafiri na kuharibu mwelekeo wao  wakati wanapohama kwenda umbali mrefu.

Siku ya ndege wanaohama duniani ni kampeni ya kila mwaka ya uhamasishaji inayolenga kuwalinda ndege wanaohama na makazi yao. 

Kampeni hii inaenea ulimwenguni kote na imekuwa chombo bora cha kusaidia kuongeza ufahamu wa kimataifa kuhusu vitisho kwa ndege wanaohama, umuhimu wao wa kiikolojia na hitaji la ushirikiano wa kimataifa kuwalinda. 

Siku ya ndege wanaohama duniani huadhimishwa mara mbili kwa mwaka Mei 15 na Oktoba 8.

Mwangaza bandia huua mamilioni ya ndege kila mwaka

Kila mwaka, taa za bandia husababisha vifo vya mamilioni ya ndege. Unabadilisha mifumo ya asili ya mwanga na giza katika mifumo ya ikolojia, ambayo huathiri mifumo ya uhamaji wa Ndege hao, ulishaji wa vifaranga vyao na tabia ya kuimba.

Ndege wanavutiwa na mwanga wa bandia usiku, hasa katika wingu la chini, ukungu, mvua, au wakati wa kuruka kwenye miinuko ya chini.

Lakini ndege hao wanaohama huchanganyikiwa na wanaweza kuzunguka majengo yenye mwanga. 

Ndege waliochoka na waliochanganyikiwa huwa mawindo rahisi kwa wanyama wanaowinda wanyama wengine au wanakufa kwa sababu ya kugongana na majengo sababu ya mwanga huo bandia wa taa.

Ndege wanaohamahama usiku kama vile bata, bata bukini, ndege wa ufuoni, ndege wa majini na ndege wanaoimba huteseka zaidi kutokana na mwangaza wa bandia. Mwangaza wa bandia pia huvutia ndege wa baharini kama vile petroli, ambao ni mawindo ya panya na paka.

Ndege wa Arctic msimu wa joto wa kaskazini kati ya kaskazini mwa Ufaransa, Iceland na Greenland.
Jakub Fryš

Kila mwaka kiwango cha uchafuzi wa mwangaza bandia wa taa kinaongezeka duniani. Hivi sasa zaidi ya asilimia 80 ya watu wote duniani wanaishi katika anga zenye mwangaza bandia na Ulaya n Amerika ya kaskazini inakaribia asilimia 99.

Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kwamba kiwango cha mwangaza bandia duniani kinaongezeka kwa angalau asilimia 2 kila mwaka.

Soma pia kuhusu

Siku ya ndege wanaohama: Ndege aina ya flamingo waridi walifika Nur-Sultan kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi

Giza la asili lina thamani ya uhifadhi sawa na maji safi, hewa na udongo. Lengo kuu la siku ya ndege wanaohama wuniani kwa mwaka huu ni kuongeza ufahamu wa tatizo la “uchafuzi wa mwanga na athari zake mbaya kwa ndege wanaohama,” amesema Amy Frenkel, katibu mtendaji wa mkataba wa aina zinazohama za wanyama pori.

Amesisitiza kuwa serikali nyingi, miji, makampuni na jumuiya kote ulimwenguni tayari zinachukua hatua za kukabiliana na "uchafuzi wa mwanga". 

Miji zaidi na zaidi duniani kote inakataa kuwasha taa kwenye majengo wakati wa uhamiaji wa ndege ambao ni msimu wa wa majira chipukizi na vuli.