Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni wakati wa kuhakikisha afya ya akili kwa wote ni kipaumbele cha kimataifa:Guterres 

Mwanamke akiwa amepiga picha mbele ya mchoro unaowakilisha jua wakati wa siku ya afya ya akili duniani
UN Photo: M. Perret
Mwanamke akiwa amepiga picha mbele ya mchoro unaowakilisha jua wakati wa siku ya afya ya akili duniani

Ni wakati wa kuhakikisha afya ya akili kwa wote ni kipaumbele cha kimataifa:Guterres 

Afya

Wakati umefika wa kuhakikisha afya ya akili kwa wote inakuwa ni kipeumbele cha kimataifa amesema hii leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akikisitiza kwamba hicho ni kipaumbele chake katika Umoja wa Mataifa na anafahamu kuwa ni changamoto kubwa kote duniani kushughulikia suala la afya ya akili. Flora Nducha na taarifa kamili 

Bwana Guterres kupitia ujumbe maalum wa siku hii iliyobeba mauadhui “Kuifanya afya ya akili kuwa kipeumbele cha kimataifa” amebainisha kwamba karibu watu bilioni moja wanaishi na matatizo ya afya ya akili kote duniani lakini  “Afya ya akili inasalia kuwa moja ya maeneo yaliyopuuzwa kwa kiasi kikubwa katika huduma za afya. Baadhi ya nchi zina wahudumu wawili tu wa afya ya akili katika kila watu 100,000 na athari za kijamii na kiuchumi za janga hili ni kubwa mno.” 

Katibu Mkuu ameendelea kusema kuwa matatizo ya hofu na wasiwasi pekee yanaugharimu uchumi wa kimataida dola zinazokadiriwa kuwa trilioni 2 kila mwaka. 

Hivyo amechagiza kwamba lazima kuimarisha uwezo wa huduma za afya ili kuweza kutoa huduma zenye ubora kwa wale wanaoihitaji hususan vijana. Na amezitaja huduma hizo kuwa ni pamoja na “Huduma za kijamii na ujumuishaji wa msaada kwa masuala ya afya ya akili katika huduma za jumla za afya na za kijamii. Kuwekeza katika afya ya akili inamaanisha kuwekeza katika afya na ustawi wa jamii. Ni lazima tushughulikie pia unyanyapaa na ubaguzi na kumaliza vikwazo ambavyo vinawazuia watu kupata huduma na msaada, na lazima pia tuzuie mizizi ya matatizo ya afya ya akili ikiwemo machafuko na unyanyasaji” 

Bwana Guterres amehitimisha ujumbe wake kwa ahadi kwamba Umoja wa Mataifa umejizatiti kufanyakazi na wadau kuchagiza masuala ya afya ya akili. 

Ametoa wito kwa dunia kwamba wati wa kuadhimisha siku hii hebu waifanye afya ya akili kuwa kipaumbele cha kimataifa na kudchukua hatua haraka ili kila mtu , kila mahali aweze kupata fursa ya huduma bora za afya ya akili. 

Siku ya afya ya akili duniani huadhimishwa kila mwaka Oktoba 10. 

 

TAGS: Siku za UN, afya ya akili,