Haiti hali si shwari, viwango vya juu zaidi vya njaa vyaripotiwa kwa mara ya kwanza
Msururu wa majanga yasiyo na huruma yanazidi kukumba wananchi wa Haiti kila uchao na kusababisha taifa hilo kuwa katika mkwamo,yameonya mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa lile la chakula na kilimo duniani, FAO na la mpango wa chakula duniani, WFP kupitia taarifa yao waliyoitoa leo hii kutoka mji mkuu wa Haiti, Port- au- Prince. Mashirika hayo yanasema nusu ya wananchi wa Haiti wanakabiliwa na uhaba mkubwa zaidi wa chakula.