Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utabiri wa ukuaji wa kiuchumi mwaka 2023 wapungua kutoka asilimia 3 mpaka 1.9

Makonteina katika bandari moja yakionyesha kuimarika kwa uchumi
Photo: Dominic Sansoni/World Bank
Makonteina katika bandari moja yakionyesha kuimarika kwa uchumi

Utabiri wa ukuaji wa kiuchumi mwaka 2023 wapungua kutoka asilimia 3 mpaka 1.9

Ukuaji wa Kiuchumi

Benki ya Dunia imepunguza utabiri wake wa ukuaji wa uchumi kwa 2023 kutoka asilimia 3 hadi asilimia 1.9, nakusema dunia iko karibu na mdororo wa uchumi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Washington DC nchini Marekani Rais wa Benki ya Dunia David Malpass amesema ofisi yake inatetea nchi kuwa na majibu yaliyolenga kuwasaidia masikini na ameonyesha wasiwasi wake kuwa kwa kuendelea kuwa kushuka mapato ya wastani ya kimataifa kutazidisha vikwazo vya mitaji kufikia nchi zinazoendelea kiuchumi.

“Tumepunguza kiwango cha ukuaji, tumepunguza utabiri wetu wa ukuaji kwa mwaka 2023 kutoka asilimia 3 hadi asilimia 1.9 kwa ukuaji wa kimataifa. Hii ni hatari karibu na mdororo wa uchumi wa dunia na kwamba mdororo wa kiuchumi unaweza kutokea wakati fulani. “

Malpass amesema matatizo yote ambayo watu wameyazingatia kwa sasa kama vile tatizo la mfumuko wa bei, kiwango cha riba kupanda na kupungua kwa mitaji kwa nchi zinazoendelea kunawaathiri zaidi maskini na hivyo ni changamoto kubwa kwa Benki ya Dunia.

“Baadhi ya nchi tayari zimekuwa zikipandisha viwango vyao vya riba na huenda sasa zinafikia hatua ambayo hazihitaji kuendelea kuongeza. Baadhi ya nchi zimefanya zimetoa .” Ameongeza kuwa  ni muhimu sana, “nchi zingine ni wazalishaji wa bidhaa na zingine ni wanunuzi wa bidhaa. Kwa hivyo kwa ujumla tumetetea nchi ambazo zinaposhughulikia mzozo huo, zijaribu kuwa na majibu yaliyolenga pande zote ikimaanisha msaada kwa maskini, kuingiliaji kati na pia kuna na mkakati wa kutoka katika dimbi hili la hali ngumu na kuwa hali hii ni ya muda mfupi.”

Pesa zinazotumwa na wafanyakazi wahamiaji wa ng'ambo kwa nchi zao zinazidi kuwa muhimu kwa familia na uchumi mpana
IOM/Muse Mohammed
Pesa zinazotumwa na wafanyakazi wahamiaji wa ng'ambo kwa nchi zao zinazidi kuwa muhimu kwa familia na uchumi mpana

Tunataka kusaidia watu wote

Benki ya Dunia imeeleza dhamira yake ya kuhakikisha kuna ustawi wa pamoja wa uchumi na kwamba wangependa kuona nchi zinazoendelea na zilizoendelea zote uchumi wake ukiimarika na kwamba uwepo wa mdororo wa kiuchumi inamaanisha utapunguza wastani wa mapato .

Wameeleza pia wamekuwa na wasiwasi juu ya mkusanyiko wa mitaji katika nchi zenye uchumi wa kiwango cha juu na wametaka suala hili lishughulikiwe iki nchi zinazoendelea pia ziweze kupata mitaji ya kuanzisha biashara mpya na ili kuhakikisha haya yanatokea lazima kuwepo na mabadiliko katika mwelekeo wa sera za fedha na kiuchumi kwa nchi zinazoendelea.

“Benki ya dunia tunakumbatia dhana ya jinsi gani tunaweza kupata rasilimali zaidi. Tunaelewa jinsi ilivyo muhimu kwa watu katika nchi zinazoendelea. Tumekuwa tukizungumzia ukata wa rasilimali unaotokana na mtiririko wa mitaji kutoka kwenye masoko kufungwa, kwenda nchi mbalimbali. Na kuna changamoto kubwa, naiita mgogoro katika maendeleo. Hivyo mojawapo ya suluhu ni rasilimali zaidi, ikiwa ni pamoja na rasilimali zaidi kupitia Benki ya Dunia.” Malpass aliwaambia waandishi wa habari.

Kwa sasa Benki ya Dunia ipo kwenye mkutano wa mwaka wa wanachama wake.