Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Mtazamo wa maeneo ya forodhani visiwani Zanzibar.
UN News/Assumpta Massoi

Filamu ya Royal Tour Tanzania ni mkombozi wa sekta ya utalii 

Hatimaye filamu ya Tanzania The Royal tour iliyotengenezwa kuonesha vivutio vya utalii katika taifa hilo la Afrika Mashariki imezinduliwa nchini Marekani huku Msemaji Mkuu serikali ya Tanzania akisema filamu hiyo itakuwa mkombozi wakati huu ambapo mataifa mbalimbali ikiwemo Tanzania zinahaha kujikwamua kiuchumi baada ya janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19. 

Kijiji cha Novoselivka karibu na Chernihiv, Ukraine umepigwa mabomu.
UNDP Ukraine/Oleksandr Ratushnia

Ushahidi wa uhalifu wa vita waongezeka Ukraine, haki za binadamu lazima ziheshimiwe:OHCHR

Uvamizi wa Urusi karibu miezi miwili iliyopita umeitumbukiza Ukraine katika mzozo wa haki za binadamu na janga la kibinadamu ambalo limeharibu maisha ya raia kote nchini na kwingineko, amesema leo kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu Michelle Bachelet huku akizitaka pande zote husika katika mzozo huo kuheshimu sheria za kimataifa za haki za binadamu na hasa kanuni zinazosimamia masuala ya uhasama. 

Jumba la ghorofa lililoharibiwa kufuatiwa mashambulizi wilaya ya Obolon, Kyiv, Ukraine.
© UNDP/Oleksandr Ratushniak

Robo ya watu wote nchini Ukraine wanahitaji msaada:UN 

Katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, Ukraine imeshuhudia "mateso, madhila na uharibifu kwa kiwango kikubwa", amesema mratibu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mgogoro wa Ukraine akizungumza na waandishi wa habari hii leo mjini Lviv Msagharibi mwa Ukraine, na kumuunga mkono Katibu Mkuu kwa kusema, "lazima tukomeshe umwagaji damu na Uharibifu  nchini humo". 

Familia za Turkana zinatumia kilimo cha umwagiliaji kulima mazao ya chakula wakati wa ukame wa muda mrefu nchini Kenya.
UNDP/Ngele Ali

Mradi wa FAO na WFP wawanusuru wakulima walioathirika na mabadiliko ya tabianchi Kenya 

Kutana na Agnes mkulima kutoka wilaya ya Lodwar kaunti ya Turkana jimbo la Rift Valley nchini Kenya. Mabadiliko ya tabianchi yanayolikumba eneo la Afrika Mashariki kwa kiasi kikubwa yamemuathiri sana yeye na jamii yake, lakini sasa asante kwa mradi wa pamoja wa mashirika ya Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP na la chakula na kilimo FAO wa kuwasaidia wakulima wadogo kujenga mfereji wa maji kwa ajili ya umwagiliaji na kununua mazao yao, maisha ya Agnes na jamii yake yamebadilika.

Sauti
2'36"