Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Safari ya lori kuelimisha jamii kuhusu COVID-19 imenifunza mengi:Ntlabati 

Lori lililoratibiwa UNICEF Afrika Kusini na idara za afya za nchi hiyo limekuwa likionyesha video na kutoa matangazo ya watu kuelezea hadithi zao kuhusu COVID-19 kote Afrika Kusini kwa kutumia lugha yao ya mama na kuhamasisha ujumbe wa kupokea chanjo
© UNICEF South Africa

Afya

Pumla Ntalabati ni mfanyakazi mshauri wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Afrika Kusini, anasema janga la corona au COVID-19 limemfundisha za mengi, kuanzia amri ya watu kusalia majumbani hadi safari yam ilima na mabonde ya kuelimisha umma katika jimbo la Kwazulu Natal kwa kutumia usafiri wa lori la magurudumu 18. 

Imekuwa ni muda mrefu tangu tangu nilipofanya safari yoyote binafsi na sababu kubwa ni janga la corona au COVID-19 ambalo limeitikisa dunia nzima na linaendelea kusababisha madhila kila kona anasema Ntalabati 

“Kwa kweli, janga la COVID-19 linafaa kulaumiwa ulimwenguni kote kwani lililazimisha maisha yangu kutiwa kufuli kwa mud ana kusalia nyumbani tu hali iliyochosha mwili na akilini.” 

Lkini wakati nilifanya uamuzi wa kuiacha ofisi yangu ya nyumbani Johannesburg na kuelekea mkoa wa KwaZulu-Natal (KZN) nilikuwa na hisia tofauti.  

Ingawa nilikuwa na furaha ya kujerea katika ngoma inayoijua ya kazi yangu ikinikumbusha pia wakati wangu kama mtafiti, wakati nilipoweza kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine na kutoka kijiji hadi kijiji ilikuwa kitu rahisi , lakini sasa nina hofu na mashaka kiasi kana kwamba ni siku ya kwanza navaa za shule wakati nikitoka nje ya mlango wangu wa mbele ya nyumba yangu. 

Lakini niliamua kufanya hivyo sababu naipenda kazi yang una kwa vilima vilivyo tamalaki kijani kibichi na anga zilizojaa mawingu za Kwazulu Natal na watu wake.  

Jimbo hilo lina kila kitu kijani kibichi kisicho na mwisho, mwendo mrefu kwenye uwanja mkubwa, mtindo wa maishawa polepole, Bahari ya Hindi yenye maji ya uvuguvugu, hewa yenye unyevu na nguvu na msisimuko  mkubwa kila unapogeukia.iko kila mahali unapogeuka. 

Hilo ndilo lililonifanya mimi na wenzangu kuingia kwenye Ndege mara tu viwanja vilipofunguliwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa King Shak ana kunikumbusha jukumu kubwa tulilonalo katika jamii. 

“Na tuko hapa kukutana la lori kubwa la magurudumu 18, lori la aina yake ambalo masuala ya Habari na mawasiliano, lori ambalo limechanja mbuga za kila kona ya miji, vijiji na vitongoji vya Afrika Kusini ili kuhakikisha jamii zinapata Habari na maendeleo ya ugonjwa wa COVID-19 kupitia ujumbe rahisi lakini maalum.” 

Lori lililoratibiwa UNICEF Afrika Kusini na idara za afya za nchi hiyo limekuwa likionyesha video na kutoa matangazo ya watu kuelezea hadithi zao kuhusu COVID-19 kote Afrika Kusini kwa kutumia lugha yao ya mama na kuhamasisha ujumbe wa kupokea chanjo
© UNICEF South Africa/Dlamini

Lori hili nichombo kilichobeba ujumbe kwa kutumia magurudumu yake linaufikisha katika kila mitaa ili wananchi waelewe jinsi COVID-19 ilivyoathiri maisha ya watu kwa lengo la kuongeza uelewa wa jinsi ya kuzuia COVID-19 pikiwa ni pamoja na kuchukua hatua mbalimbali kama vile kunawa mikono, kuvaa barakoa na kuzingatia umbali wa kijamii.  

Hii ni kampeni ya UNICEF na inasaidia juhudi za idara za afya za mikoa na inaambatana na timu zilizopata mafunzo za ushiriki wa jamii mashinani kwa lengo la kujenga uelewa zaidi na kuongeza ufikiaji wa huduma za kawaida za afya kama uchunguzi wa kifua kikuu au TB na virusi vya ukimwi VVU, upimaji wa shinikizo la damu na upimaji wa COVID-19. 

Wakati utoaji wa chanjo Afrika Kusini unashika kasi, lori pia linatumika kama chanzo muhimu cha habari zinazoaminika kwa kushughulikia kero za watu na kuwachagiza kuzingatia ujumbe wa wazi, wa msingi na wa ukweli.  

Timu za afya za mikoa na vijana wa kujitolea wa UNICEF sasa wanaandamana na lori hili kusaidia kusajili wazee wa umri wa zaidi ya miaka 60 kwa ajili ya chanjo. 

“Mimi na wafanyakazi wenzangu tulipowasili katika maduka makubwa ya Esikhawini karibu saa mbili na nusu kwa gari kutoka Kaskazini mwa Durban tulishuhudia mashamsham, na mirindimo katika uwanja wa kuegesha magari” 

Lori lililoratibiwa UNIVCEF Afrika Kusini na idara za afya za nchi hiyo limekuwa likionyesha video na kutoa matangazo ya watu kuelezea hadithi zao kuhusu COVID-19 kote Afrika Kusini kwa kutumia lugha yao ya mama na kuhamasisha ujumbe wa kupokea chanjo
© UNICEF South Africa/Hartford

"Jiunge na timu yangu, jiunge na chanjo!", Sauti inasikika hata ukiwa mbali na pia kwenye teksi na ujumbe kuwafikia wanunuzi waliokuwa katika haraka wa kununua bidhaa za kumaliza mwezi.  

Na sauti hiyo ndiyo iliyosikika kwenye lorim letu pia kupitia sauti ya mmoja wa waliohojiwa, ukifuatana na maandishi makubwa kwenye skrini pamoja na maandishi ya mkalimani wa lugha ya ishara ambaye alikuwa akiwasilisha ujumbe huo huo. 

Watu walisimama, wakiwa na mifuko yao pembeni, walitazama na kuuchukua ujumbe huo na hilo ndio lilikuwa lengo letu kubwa.  

Wachache walitingisha vichwa vyao na kulalamika kuwa COVID-19 ni "ugonjwa wa matajiri," au kwamba janga hilo ni mkakati wa kupunguza idadi ya watu na ni kazi ya wasomi wa ulimwengu huu.  

Lakini wengi waliojitokeza kuzungumza na wauguzi na wahudumu wa afya wanaotoa huduma waliuliza ikiwa wangeweza kupatiwa chanjo, hapo hapo. 

Lori liligundua wasiwasi na hofu ya watu kuhusu COVID-19 na chanjo kila mahali lilipokwenda.  

“Uvumi na nadharia za kula njama ziliwekwa mbele pamoja na wasiwasi wa kweli juu ya usalama na ufanisi wa chanjo na, muhimu zaidi, ombi la kujua ukweli. Katika visa vyote, wafanyikazi na huduma ya afya waliweza kutoa habari sahihi na kukanusha uwongo na kuweka bayana ukweli.” 

Lori lililoratibiwa UNICEF Afrika Kusini na idara za afya za nchi hiyo limekuwa likionyesha video na kutoa matangazo ya watu kuelezea hadithi zao kuhusu COVID-19 kote Afrika Kusini kwa kutumia lugha yao ya mama na kuhamasisha ujumbe wa kupokea chanjo
© UNICEF South Africa/Dlamini
Lori lililoratibiwa UNICEF Afrika Kusini na idara za afya za nchi hiyo limekuwa likionyesha video na kutoa matangazo ya watu kuelezea hadithi zao kuhusu COVID-19 kote Afrika Kusini kwa kutumia lugha yao ya mama na kuhamasisha ujumbe wa kupokea chanjo

Kwa kulenga “maeneo yenye maeneo ya mikusanyiko” kama vile vituo vya usafiri na vituo vya ununuzi, uwepo wa lori uliinua hamasa na mahali hapo, ikipunguza wasiwasi wa kutoweza kufanya sherehe baada ya karibu mwaka mmoja wa watu kufungiwa majumbani mfululizo. 

Wakati ulipofika wa kuendelea mbele na safari , timu ya lori na mimi tulighubikwa na maombi ya kuongeza vituo zaidi vya kuhamasisha.  

Ilipowezekana, lori lilichukua njia za kupitia vitongoji na barabara kuu ili kukidhi maombi haya. 

"Uzuri wa lori ni kwamba ni suluhisho la mawasiliano lisilo la kuruhusu watu kukaribiana na hivyo kuzingatia masharti ya COVID-19 ya kukaa umbali wa mita 6 na pia linaweza kufika mahali watu walipo na kuzungumza nao kwa lugha zao," amesema mwenzetu na mratibu wa lori, Fungayi Kanyuchi. 

Lori lililoratibiwa UNICEF Afrika Kusini na idara za afya za nchi hiyo limekuwa likionyesha video na kutoa matangazo ya watu kuelezea hadithi zao kuhusu COVID-19 kote Afrika Kusini kwa kutumia lugha yao ya mama na kuhamasisha ujumbe wa kupokea chanjo
© UNICEF South Africa/Hartford
Lori lililoratibiwa UNICEF Afrika Kusini na idara za afya za nchi hiyo limekuwa likionyesha video na kutoa matangazo ya watu kuelezea hadithi zao kuhusu COVID-19 kote Afrika Kusini kwa kutumia lugha yao ya mama na kuhamasisha ujumbe wa kupokea chanjo

Ambapo wengi hawaamini chanjo na asili ya janga ya virusi bvya corona, kuzungumza kwa Kiingereza wakati mwingine kunaweza kuzidisha hisia hizi. Kushuhudia watu wakisimamaz kutazama video zinazochezwa kwa lugha yao ya kienyeji, ya kiZulu kwenye jimbo la Kwazulu Natal, uwezo wa lori hilo kufikisha ujumbe ambao uliwaingia kweli watu wa eneo hilo ilikuwa bayana. 

Baada ya siku sita barabarani lori likaelekea kwenye jimbo la Kaskazini-Magharibi kwenda kluisaidia idara ya afya kuendfesha kampeni kama hii tena.  

 Kwa kadiri nilivyokuwa nimesahau jinsi ilivyokuwa kusafiri, nilikuwa pia nimesahau hisia ya furaha ambayo inakuja na kushuhudia athari za kazi yetu.