Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Watoto wakiwa wamevalia barakos kwenye shule katika kambi ya Far'a ya wakimbizi huko West Bank.
© UNRWA/Kazem Abu Khalaf

Ingawa tunalazimika kuvaa barakoa lakini hatupaswi kufungwa midomo:Watoto

Leo ni siku ya watoto duniani maudhui yakiwa "kutafakari dunia bora kwa kila mtoto", na watoto kutoka kila kona ya dunia kupitia shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, wameandika shairi kufikisha ujumbe muhimu kwa viongozi wa dunia hii, wazazi na jamii wakitaka sauti zao zisikike na hatua zichukuliwe kulinda kizazi hiki na vijavyo.

Sauti
1'58"
Mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros Ghebreyesus akizungumza katika moja ya taarifa za WHO kuhusu janga la COVID-19
UN Photo/Evan Schneider

Ninaumia kwa kinachoendelea nyumbani Ethiopia siwezi kuegemea upande wowote:Dkt.Tedros 

Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema anaumia na kupata uchungu mkubwa moyoni kufuatia hali ya machafuko inayoendelea Ethiopia nchi anakotoka ,na amertoa wito kwa pande zote katika mzozo kufanya kila liwezikanalo kwa ajili ya kurejesha amani na kuhakikisha ulinzi wa raia na pia kutoa fursa za huduma za afya na misaada ya kibinadamu kwa wale wanao ihitaji. 

Picha ya maktaba ikionesha wachimba dhahabu nchini Ghana.
Picha: IRIN/John Appiah

Niliona Kijiji chetu kina watu wawili tu waliosoma, nikaingia kwenye migodi kutafuta pesa-Lawrence  

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linaendelea kushirikiana na Serikali ya Uganda, sekta binafsi na washirika wengine kuhamasisha makampuni na wadau wote kuhusu haki za watoto na pia katika shughuli zao za kila siku, kuwa na sera rafiki za watoto. Hiyo ni kutokana na watoto wengi kutumikishwa katika shughuli mbalimbali za kiuchumi badala ya kuwa shuleni kama anavyoeleza mtoto Lawrence katika taarifa hii inayosimuliwa na Anold Kayanda. 

Sauti
2'18"
Wauguzi wakisherekea  mwisho wa janga la Ebola mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo wafanyakazi zaidi ya 200 walifanya kazi bila kuchoka kulinda watoto kutokana na ugonjwa huo.
© UNICEF/Jean-Claude Wenga

UNICEF: Ebola kwaheri katika jimbo la Equateur DRC 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF leo limekaribisha tangazo la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, linalothibitisha kumalizika kwa mlipuko wa karibuni wa Ebola katika jimbo la Equateur Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.

Sauti
1'37"