Guterres akaribisha mdahalo wa kitaifa baina ya serikali na asasi za kiraia Nicaragua
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amekaribisha mdahalo wa kitaifa baina ya asasi za kiraia, viongozi wa dini na serikali kufuatia machafuko baina ya vikosi vya ulinzi na raia katika taifa la Nicaragwa mwezi April.