Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki za wanawake Sudan zinatutia mashaka:UN

UN Photo - Jean-Marc Ferre
Ravina Shamdasani, msemaji wa ofisi ya haki za binadamu Geneva. Picha:

Haki za wanawake Sudan zinatutia mashaka:UN

Haki za binadamu

Ubaguzi na ukatili ikiwemo ukatili wa kingono dhidi ya wanawake na wasichana nchini Sudan umefanya macho yote ya ulimwengu kuikodolea nchi hiyo hasa kutokana na kesi ya msichana Noura Hussein Hammad Daoud.

Kauli hiyo imetolewa leo na ofisi ya haki za binadamu mjini Geneva Uswis kufuatia Binti Noura kuhukumiwa kifo wiki iliyopita na mahama moja nchini Sudan baada ya kumchoma kisu na kumuua mumewe ambaye alilazimishwa kuolewa naye na kudaiwa kubwa mara kwa mara na bwana huyo.

Ravina Shamdasan ni msemaji wa ofisi hiyo ya haki za binadamu ambaye amewaambia waandishi wa habari ya kwamba Tuimepokea taarifa kwamba ndoa ya shuruti ya bi Hussein, kubakwa na mifumo mingine ya ukatili wa kijinsia dhidi yake havikupewa uzito na mahakma kama ushahidi kwenye hukumu ya kesi hiyo, na kwamba hakikisho la kutendeka haki katika kesi hiyo halikutekelezwa , na sababu kesi hiyo imepata umaarufu mkubwa wa kimataifa tunahofia usalama wake, wa mawakili wake na wengine wanaomuunga mkono.”

Ofisi ya haki za binadamu imeutaka uongozi wa Sudan kuhakikisha ulinzi wa kimwili na kisaikolojia wakati Noura akiwa mahabusu , lakini pia kuheshimu haki zake za kuwa na haki katika kesi hiyo na kuweza kukata rufaa.

Naye mwakilishi malumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya mauaji amesema kwamba kumuhukumu kifo wakati kukiwa na ushahidi dhahiri wa kulinda maisha yake alipotekeleza kosa hilo , itakuwa ni mauaji ya kiholea dhidi ya binti huyo hasa ukizingatia kwamba wanawake wengi wamekuwa wakihukumiwa kwa mauaji kutokana na kujilinda dhidi ya maisha yao, na hivyo ameitaka serikali ya Sudan kuyapa uzito madai ya Noura ya kujilinda dhidi ya jaribio la mumewe kutaka kumbaka tena.

Marekebisho ya vifungu vya sheria vya makossa ya jinai nchini Sudan yalifanyika mwaka 2015 , lakini bado makossa ya ukatili majumbani na ubakaji katika ndoa hayajaharamihwa na sharia hizo.