Joto kali latarajiwa msimu wa kiangazi mwaka huu:WMO

18 Mei 2018

Joto kali linatarajiwa katika msimu wa kiangazi mwaka huu 2018 kuanzia  Juni, Julai na Agosti, huku theluji katika maeneo ya Arctic ikiwa chini ya kiwango cha kawaida.

Mtazamo huu ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo na shirika la kimataifa la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO baada ya kumalizika mkutano juma hili mjini Ottawa Canada uliokuwa ukiangalia mtazamo wa hali ya hewa na mwelekeo katika maeneo ya Arctic, ikiwa ni mara ya kwanza mkutano huo kufanyika.

Kwa mujibu wa WMO lengo kuu la ripoti hii ni kutoa hali halisi ya kinachotarajiwa ili kuweza kuboresha hali ya hewa, mazingira na kulinda theluji katika ukanda ambao unakumbwa na mabadiliko ya haraka ya kimazingira.

WMO inasema kwa miaka mitatu mfululizo kiwango cha joto duniani kimekuwa cha juu , huku katika baadhi ya maeneo kukikumbwa na ukame wa kupindukia, mafuriko, na hata vimbunga vilivyosababisha hasara kubwa kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter