Maboya chakavu yageuzwa mabegi ya gharama
Maboya yamekuwa yanatumika kusafirishia wakimbizi na wasaka hifadhi. Mara nyingi maboya haya yanapotia nanga huko Ulaya huwa yamechakaa na hivyo kutupwa kiholela. Hivi sasa wasichaan wawili huko Ujerumani wamegeuza taka hizo kuwa bidhaa ya aina yake.