Guterres alaani mashambulizi dhidi ya nyumba za ibada Indonesia
Amani na Usalama
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia msemaji wake amelaani mashambulizi ya kigaidi dhidi ya waumini kwenye nyumba za ibada 3 hii leo katika mji wa Surabaya Indonesia na kukatili maisha raia wasio na hatia na kujeruhi wengi.
Kupitia msemaji wake, Bwana Guterres ametuma salamu za rambirambi kwa familia za wafiwa huku akiwatakia ahueni ya haraka majeruhi.
Halikadhalika Katibu Mkuu ameonyesha mshikamano wake kwa serikali ya Indonesia katika mapambano dhidi ya makundi ya kigaidi na siasa za kichochezi za makundi ya wanamgambo.
Mkuu huyo ameitaka serikali ya Indonesia kufanya uchunguzi wa kina na kuwafikisha wahusika katika vyombo vya sheria