Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tupaze sauti katika utetezi wa ndege wahamiaji: Guterres

Ndege wahamiaji wakiwa katika safari zao kuelekea kusini.
Picha ya WMB
Ndege wahamiaji wakiwa katika safari zao kuelekea kusini.

Tupaze sauti katika utetezi wa ndege wahamiaji: Guterres

Tabianchi na mazingira

Katika maadhimisho ya siku ya ndege wahamiaji leo jijini New York Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres   ameihiza  dunia kulinda ndege wahamiaji. Kaulimbiu ya maadhimisho hao ni “kwa pamoja tupaze sauti katika utetezi na ulinzi wa ndege wahamiaji”.

Katika ujumbe wake Bwana Guterres amesema ndege wahamiaji ni ishara ya amani pia ni kiunganishi cha tamaduni ambazo kwa njia moja au nyingine   hukutanisha  jamii na husaidia katika ulinzi wa mazingira katika mataifa mbalimbali.


Pia ameongeza kuwa safari za ndege hao kutoka sehemu moja na kwenda sehemu nyingine kila mwaka huwahimiza watu wa kila rika duniani kote mienendo yao, hivyo katika maadhimisho ya leo ni fursa ya kipekee ya kusherekea uwepo wa viumbe hao, na pia ni iwe  fundisho kwetu kuweza kupigania haki ya uhai wa ndege hao ambao wana mchango mkubwa katika mazingira tunamoishi,


Kati aina 11,000  ya ndege duniani, moja kati ya watano huhesabiwa kuwa ndege wahamiaji na  asilimia arobaini kati yao wapo hatarini kutoweka. 
Vitisho vingi vinavyosababisha kutoweka kwa ndege hao duniani ni pamoja na kupoteza makazi yao na uharibifu unaosababishwa na maendeleo ya kilimo cha kisasa  kwenye maeneo ya pwani, mavuno yasiyo endelevu, na uuaji wa ndege hao kinyume cha sheria.


Bwana Guterrea ametoa wito kwa serikali mbalimbali, asasi za kiraia na mashirika ya kibinadamu duniani kwa pamoja kushirikiana katika ulinzi wa ndege wahamiaji, huku akiahidi kwamba Umoja wa Mataofa utatoa kipaumbele katika ulinzi na utetezi wa haki za ndege wahamiaji katika harakati za ulinzi wa mazingira.