Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chonde chonde Sudan ruhusuni rufaa ya Noura: UN women/UNFPA/UNOSAA

Picha:MONUSCO
Ubakaji na ukatili wa kingono ni ukiukaji wa haki za binadamu

Chonde chonde Sudan ruhusuni rufaa ya Noura: UN women/UNFPA/UNOSAA

Haki za binadamu

Aozwa kwa lazima, akatoroka  , nduguze wakamrejesha kwa nguvu kwa mumewe ambaye alimbaka, na kwa kushindwa kuvulia hilo akamchoma kisu mumewe na kumua, sasa Noura hassan kutoka Sudan anakailiwa na hukumu ya kifo, mashirika ya Umoja wa Mataifa, raia wa sudan na wanaharakati wa haki za wanawake na wasichana wanataka aruhusiwe kukata rufaa.

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yameungana na wananchi wa Sudan kuisihi serikali ya nchi hiyo kuruhusu rufaa ya kesi ya binti wa miaka 19 aliyemuua mumewe. Grace Kaneiya na tarifa kamili

(TAARIFA YA GRACE KANEIYA)

Mashirika hayo lile la masuala ya wanawake UN Women, la idadi ya watu duniani UNFPA na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya mshauri maalumu kwa ajili ya Afrika UNOSAA, kwa pamoja wametoa wito huo Jumapili kwa serikali ya Sudan wakiiomba kuruhusu kukatwa rufaa kwa kesi dhidi ya Noura Hussein mwenye umri wa miaka 19 ambaye amehukumiwa kifo kwa kukatili maisha ya mumewe.

Duru zinasema Noura alishinikizwa kuolewa akiwa na umri wa miaka 16, na baada ya muda alitoroka, lakini ndugu zake walimsaka na kumrejesha kwa mumewe aliyembaka kwa msaada wa ndugu zake watatu wa kiume  akiwemo kaka yake waliomkandamiza chini kuruhusu ukatili huo. Na mumewe alipotaka kumbaka wa mara ya pili ndipo Noura alimchoma kisu mara kadhaa na kumuua.

Alhamisi iliyopita jaji wa mahakama ya Omdurman alithibitisha hukumu ya kifo dhidi ya Noura kwa mauaji baada ya familia ya mumewe kukataa uwezekano wa kulipwa fidia na badala yake kumuomba jaji ampe hukumu ya kifo.

Mawakili wa Noura hivi sasa wana siku 15 za kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo ya kifo. Kwenye mitandao ya kijamii kampeni maalumu imezinduliwa kumuunga mkono Noura ambaye anasema alishitushwa sana na hukumu ya kifo aliyopewa.

Na mashirika hayo ya Umoja wa Mataifa yasema kama sauti ya wasicha na wanawake duniani, yanaiomba serikali ya Sudan kuokoa maisha ya Noura Hussein na kulinda maisha ya wanawake na wasichana wengine kama inavyoainisha katiba ya Umoja wa Mataifa na malengo ya maendeleo endelevu SDG’s.