Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutegemea msaada ni mtihani kwa elimu ya nchi za kipato cha chini na cha kati:Kikwete

Msichana mkimbizi akifanya mtihani shule ya msingi Moghadishu kwenye kambi ya Kakuma nchini Kenya
UNHCR/S.Otieno
Msichana mkimbizi akifanya mtihani shule ya msingi Moghadishu kwenye kambi ya Kakuma nchini Kenya

Kutegemea msaada ni mtihani kwa elimu ya nchi za kipato cha chini na cha kati:Kikwete

Utamaduni na Elimu

Hali ya kuwa tegemezi wa misaada inadumaza nchi nyingi kiuchumi na hata kijamii, ikiwemo katika maendeleo ya elimu. Sasa nchi masikini na zenye kipato cha wastani zinachagizwa kuondokana na hali hiyo ili kujikwamua na mzunguko wa umasikini ikiwemo elimu duni na jopo la kimataifa la ufadhili kwa ajili ya elimu limezindua ombi la dola bilioni moja kuzisaidia nchi hizo kuepukana na utegemezi.

Changamoto kubwa za elimu zinapatikana katika nchi zenye kipato cha chini na cha wastani na ni kutokana na kuwa tegemezi wa misaada ya wahisani kwa masuala mbalimbali ikiwemo suala la elimu sasa jopo la kamisheni ya ufadhili wa elimu imezindua ombo la dola bilioni moja kuzisaidia nchi hizo. Selina Jerobon na tarifa kamili

 

(TAARIFA YA SELINA JEROBON)

Kauli hiyo imetolewa na mmoja wa wajumbe wa jopo la kimataifa la kamisheni ya ufadhili kwa ajili ya elimu Jakaya Mrisho Kikwete.

Akizungumza na Idhaa hii mjini New York Marekani Rais huyo msataafu wa Tanzania amesema mkakati wa jopo hilo la ufadhili wa elimu ni kuhakikisha nchi nyingi hususani barani Afrika zinatoka katika kipato cha chini cha kutegemea misaada ikiwemo ya elimu na kuingia katika kipato cha wastani jambo ambalo litainua uchumi wa nchi hizo na itakuwa chachu ya kukuza pia kiwango cha elimu kwani

(SAUTI YA JAKAYA  KIKWETE )

Ameongeza hata zikifikiwa kiwango hicho haimaninishi ndio zimeshinda kabisa mtihani

(SAUTI YA  JAKAYA KIKWETE )