Wasiojulikana waliko waendelea kusakwa kufuatia mafuriko Kenya: UNICEF

11 Mei 2018

Idadi ya waliokufa kutokana na athari za mafuriko nchini Kenya  imepanda na maelfu wameachwa bila makazi wakihitaji msaada.

Kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa ynanayosaidianana na serikali ya Kenya kuwasaidia waathirika  hadi sasa idadi ya waliofariki imefikia watu132 huku   zaidi ya 311,000 wameachwa bila makazi. Lisa Kurbiel afisa habari na mawasiliano wa UNICEF Kenya  anafafanua kuhusu hali ilivyo kwa sasa hususani kwa waliopoteza maisha na waathirika wa kufurika kwa bwawa Nakuru

(SAUTI YA LISA KURBIEL)

Kwa bahati mbaya watu 44 wamearifiwa kufariki dunia na 39 kujeruhiwa katika janga hilo. Wakati vado watu wengine waliotawanywa bado hawajulikani walipo operesheni ya uokozi inaendelea, na idadi ya kaya ambazo zimeathirika ni 115, huku wanawake, wazee na watoto ndio waathirika wakubwa.”

Kuhusu msaada unaotolewa na UNICEF ameongeza

(SAUTI YA LISA KURBIEL)

“Tuko tayari kutoa msaada wowote utakaohitajika ili kuwasaidia, msaada wa kiafya, msaada wa makazi ya dharura, chakula na mahitaji mengine ya msingi.”

Mafuriko hayo ameathiri pia nchi jirani za Somalia na Ethiopia.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter