Ubunifu wa wanawake wabadili jamii zao #WorldIPDay
Ubunifu wa wanawake katika nyanja mbalimbali kuanzia mavazi, tiba na hata ufugaji sasa unadhihirisha kuwa udadisi wa kundi hilo ukijengewa uwezo, umaskini utasalia historia.
Ubunifu wa wanawake katika nyanja mbalimbali kuanzia mavazi, tiba na hata ufugaji sasa unadhihirisha kuwa udadisi wa kundi hilo ukijengewa uwezo, umaskini utasalia historia.
Wafanyakazi 10 wa kutoa misaada ya kibinadamu nchini Sudan Kusini wametoweka wakati wakiwa kwenye msafara wa kutathmini mahitaji ya kibinadammu huko Yei jimbo la Equitoria ya Kati nchini humo.
Shirika la wa Umoja wa Mataifa la usaidizi kwa wakimbizi wa Palestina UNRWA limesema lina wasiwasi kuhusu mgogoro wa kivita unaondelea kando mwa kambi ya wakimbizi wa Kipalestina ya Yarmouk.
Wanafunzi 56,000 kutoka shule 100 za eneo la Karamoja, kaskazini-mashariki mwa Uganda sasa hawatokuwa na hofu tena ya magonjwa yatokanayo na ukosefu wa maji safi na salama kufuatia makubaliano ya Umoja wa Mataifa na Korea Kusini.
Wafanyakazi 10 wa kutoa misaada ya kibinadamu nchini Sudan Kusini wametoweka wakati wakiwa kwenye msafara wa kutathmini mahitaji ya kibinadammu huko Yei jimbo la Equatoria ya Kati nchini humo.
Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein amehitimisha ziara yake nchini Ethiopia na kusema licha ya changamoto na misukosuko waliyopitia raia wa nchi hiyo kuna matumaini ya mambo kutengamaa.
Utafiti mpya wa Umoja wa Mataifa na wadau wake umebaini kuwa bidhaa yoyote ile inapobandikwa lebo inayoonyesha eneo halisi ilikozalishwa, inakunwa na manufaa zaidi ya kiuchumi na kijamii kwa maeneo ya kijijini na pia huchagiza maendeleo endelevu.
Mionzi ya nyuklia kutoka kinu cha Chernobyl bado inaonyesha makali yake kwa maisha ya binadamu.
Baada ya mashauriano na mazungumzo na pia kusikia kauli kutoka kwa wawakilishi wa wananchi wa Syria, wahisani wamefungua pochi zao na kuchangisha fedha kukuwamua wananchi hao ambao mustakhabali wao uko mashakani.
Hatimaye wachunguzi kutoka shirika la kuzuia silaha za kemikali, OPCW wameweza kufika eneo la pili huko Douma nchini Syria kunakodaiwa kutumika silaha za kemikali wakati wa shambulio tarehe 7 mwezi huu wa Aprili.