Skip to main content

Ikiwa na lebo ya pilipili ya Penja hutoacha kununua- FAO

Pilipili hoho inaweza kukuzwa katika mazingira tofauti
Picha ya IFAD
Pilipili hoho inaweza kukuzwa katika mazingira tofauti

Ikiwa na lebo ya pilipili ya Penja hutoacha kununua- FAO

Ukuaji wa Kiuchumi

Utafiti mpya wa Umoja wa Mataifa na wadau wake umebaini kuwa bidhaa yoyote ile inapobandikwa lebo inayoonyesha eneo halisi ilikozalishwa, inakunwa na manufaa zaidi ya kiuchumi na kijamii kwa maeneo ya kijijini na pia huchagiza maendeleo endelevu.

Lebo ya eneo la kijiigrafia au GI hutaja eneo ilipozalishwa bidhaa mathalani pilipili ya  bonde la Penja nchini Cameroon ambayo tayari imejipatia umaarufu, na huelezea ubora na ladha kulingana na eneo hilo na hata utamaduni wa eneo hilo.

 

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO pamoja na wadau wake wamesema taarifa hizo husababisha mnunuzi kuwa tayari kununua bidhaa ya aina hiyo kwa bei ya juu kwa kuwa anatambua ilikotoka, wakisema bidhaa za aina hiyo zinaweza kuchagiza thamani  ya biashara kwa zaidi ya dola bilioni 50 kwa mwaka.

 

Florence Tartanac, ambaye ni afisa mwandamizi kutoka FAO amesema Utafiti huo ulihusisha bidhaa tisa ambazo tayari zimepatiwa lebo hizo za kijiografia, ikiwemo pilipili hiyo ya Penja kutoka Cameroon na kabeji ya Futog kutoka Serbia.

 

(Sauti ya Florence Tartanac)

“Usajili wa GI uliongeza bei ya bidhaa zote tisa ambazo tulitafiti. Kwa hiyo ongezeko la thamani kutokana na GI ni tofauti katika bidhaa zote lakini kwa ujumla ongezeko lilikuwa kati ya asilimia 20 hadi 50.”

 

Bi. Tartanac lebo za kijiografia zinachochea maendeleo endelevu kwa kuwa zinaleta pamoja wakulima na wafungashaji wa bidhaa hiyo na wanakubaliana jinsi ya kudhibiti uzalishaji na hivyo kujihakikishai kipato na kutunza nembo yao biashara isinakiliwe.