Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashambulizi dhidi ya Wapalestina lazima yakome: Krähenbühl

Umati wa watu wakisubiri misaada katika kambi ya Kipalestina ya Yarmouk katika mji mkuu wa Syria Damascus mwaka 2014. Picha: UNRWA

Mashambulizi dhidi ya Wapalestina lazima yakome: Krähenbühl

Amani na Usalama

Shirika la  wa Umoja wa Mataifa la usaidizi kwa wakimbizi wa  Palestina UNRWA limesema lina wasiwasi kuhusu mgogoro wa kivita unaondelea kando mwa kambi ya wakimbizi wa Kipalestina  ya Yarmouk.

Kamishina mkuu wa UNRWA, Pierre Krähenbühl amesema  hofu yao kubwa ni kuhusu hatima ya maelfu ya wakimbizi katika kambi hiyo baada ya kuzuka mapigano mapya yaliodumu takribani wiki moja kando mwa kambi hiyo kusababisha vifo na majeruhi eneo la Yelda, ambako inasadikiwa kuwa hadi sasa watu wengi wamezingirwa bila msaada wowote.

Kwa mujibu wa UNRWA, mashambulizi ya mabomu yameathiri miundombinu ikiwemo maji, barabara na huduma za afya ambapo hospital ya Yarmouk inasadikiwa kufungwa.

UNRWA, imetoa wito kwa pande zote kinzani katika mzozo kukomesha mapigano ili kuokoa maisha maelfu ya wakimbzi  na pia kuruhusu misaada ya kibinadamu kuweza kuwafikia waathirika wa machafuko hayo ambao wengi ni wanawake, wazee na watoto.